Home SPORTS YANGA YAAHIDI KUICHAPA NAMUNGO KWAO

YANGA YAAHIDI KUICHAPA NAMUNGO KWAO

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na:Mwandishi wetu

UONGOZI wa yanga umesema kuwa kikosi chao kimejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo dhidi ya Namungo.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani jumamosi dhidi ya Namungo katika mchezo utakaopigwa dimba la  Ilulu, Lindi.

Akizungumza  jana katika kipindi kimoja cha radio, Afisa  habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hana shaka na timu pinzani kwani kikosi kimejipanga vyema kuhakikisha wanapata ushindi.

Ameongeza kuwa Namungo ni timu kubwa ambayo huwa inatoka sare  dhidi yao lakini wamepanga kuvunja huo mwiko siku ya jumamosi.

“Namungu ni timu bora na ndio maana imekuwa inatoka sare na Yanga lakini sasa tumejipanga kuhakikisha tunavuna point 3 dhidi yao licha ya kutoka sare mara nyingi” alisema.