Home SPORTS DKT ABBASI: TANZANIA NA TAIFA STARS TUNAJAMBO LETU, NJOONI KWA MKAPA

DKT ABBASI: TANZANIA NA TAIFA STARS TUNAJAMBO LETU, NJOONI KWA MKAPA

 

Serikali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wengine leo wamehamasisha watanzania kuiunga mkono Taifa Stars katika michezo yake ijayo dhidi ya DRC na Madagascar na pia kuwaunga mkono Timu ya Taifa ya Walemavu ya Soka mwenyeji wa mashindano ya Afrika hapa nchini yatakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano na wanahabari Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Timu hiyo.

Kuhusu kwenda Madagascar Serikali na Kamati ya Kuhamasisha Taifa Stars, Dr. Abbasi amesema watakodi ndege aina ya AirBus.

Kuhusu Mashindano ya Walemavu Serikali iko nao katika maandalizi na itatoa zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 135 kugharamia Timu yetu na nchi 16 zinazokuja kwa malazi, chakula na usafiri wa ndani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema kambini kuna utulivu mkubwa na hakuna tatizo lolote na pia ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha Timu inajiandaa vyakutosha.

Previous articleSEKTA YA MADINI TANZANIA YAWAVUTA WASHIRIKI EXPO 2020 DUBAI
Next articleVODACOM TANZANIA PLC WAKABIDHIWA TUZO KINARA SEKTA BINAFSI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here