Home LOCAL KANISA ANGLIKANA TANZANIA DAYOSISI YA RUVUMA LAOMBA SERIKALI KUITAZAMA HOSPITALI YA MT....

KANISA ANGLIKANA TANZANIA DAYOSISI YA RUVUMA LAOMBA SERIKALI KUITAZAMA HOSPITALI YA MT. ANNA LIULI.


Na: Maiko Luoga  Ruvuma.

Serikali nchini Tanzania inaombwa kuunga mkono juhudi za Kanisa Anglikana katika kujenga jamii iliyo bora kiafya kwa kuitazama Hospitali ya mtakatifu Anna anayomilikiwa na kanisa hilo iliyopo Liuli Halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu, uhaba wa madawa na vifaa tiba pamoja na upungufu wa watumishi wa Hospitali hiyo huku ikitegemewa na wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.

Wito huo umetolewa na Baba Askofu  Raphael Reuben Haule wa Kanisa Anglikana Tanzania dayosisi ya Ruvuma kabla ya uzinduzi wa mfuko wa kuboresha huduma ya Hospitali hiyo katika Jubilei ya miaka 50 ya Kanisa hilo iliyofanyika Oktoba 11/2021 katika Kanisa la msalaba matakatifu Liuli wilayani Nyasa.


“Kutokana na gharama za uendeshaji wa taasisi zetu hasa Hospitali ombi letu kwa serikali kuendelea kuunga juhudi za kanisa katika kujenga jamii iliyo bora kiafya, tunaiomba Serikali iitazame hospitali yetu ya mtakatifu Anna kama vile inavyotazama hospitali zake za serikali” alisema Baba Askofu Raphael Haule.

Aliongeza kuwa “Sisi tunahitaji mtusaidie madawa kuleta madaktari na kulipa mishara ya hawa madaktari kwasababu kanisa sisi peke yetu hatuwezi, Tunajua serikali inao mzigo wa taasisi zake za afya lakini hii Hospitali ya mtakatifu Anna ni sehemu ya wananchi wenu”

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mfuko huo ulioambatana na uchangiaji wa fedha, Said Omary Mailon ambaye ni mtendaji wa kata ya Liuli kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nyasa Kanali Thaomas Labani, Amepongeza mpango wa kanisa katika kuzindua mfuko huo wenye lengo la kuisaidia hospitali huku akitoa wito kwa wananchi na waumini wa kanisa hilo kuendelea kujitolea katika michango ili kuboresha hosptali hiyo.

“Kweli ukienda kwenye eneo la hospitali yetu utakuta hali sio nzuri sana lakini kumbe watu tupo na hapa nimeshuhudia naamini tutaijenga hospitali yetu, serikali haina uwezo wa kutoa fedha katika kila eneo lakini kwa umoja wetu na fikra zetu tukiweza kuchangia hata elfu kumi zitaweza kusaidia kupunguza changamoto za hospitali” alisema Said Omary Mailon.

Aidha amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa ili kufanikisha shughuli zote zinazofanywa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Nyasa na tarafa ya Liuli kwa ujumla.

Cherls Mbunda ni padre wa kanisa hilo mtaa wa Wambaguu dinari ya Mbinga na Roda Ndomba ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo walioshiriki katika misa ya jubilee ya miaka 50 ya kanisa na uzinduzi wa mfuko maalum kwa ajili ya koboresha hospitali, wamesema waumini wa kanisa hilo kwa pamoja wamekubaliana kushirika katika michango ili kusaidia hospitali.

“Mapandre wote tumekubali na tumeahidi kuchangia shilingi elfu hamsini kwa mwaka kwa kila Pandre, walei elfu hamsini lakini na watu wa kawaida shilingi elfu tano kwa kila mwaka ili kuboresha Hospitali yetu” alisema Mbunda.

Aidha waumini wa kanisa hilo wamesema wanaamini michango hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo yanayoikabili hospitali huku wakiomba waumini wote na wananchi kuona umuhimu wa mchango huo kwa ustawi wa afya za watu wa Liuli na mkoa wa Ruvuma.

Previous articleMECHI YA SIMBA NA POLISI YASOGEZWA MBELE
Next articleCAF YAIPIGA YANGA FAINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here