KIKOSI cha Yanga leo kinatua dimbani dhidi ya Geita Gold katika mchezo utakaopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kikosi hicho kitawakosa baadhi ya wachezaji katika mchezo huo.
kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari , Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani lakini wapo tayari licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji.
Pia Tonombe Mukoko ambaye ni kiungo huyu alikosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba pia aliwakosa Kagera Sugar na leo anakamilisha mchezo wake wa tatu kwa kuwa alikuwa na adhabu ya kadi nyekundu alionyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Simba katika Kombe la Shirikisho.
Pia wapo wale ambao wapo kwenye program maalumu ambao ni Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha pamoja na Dickson Ambundo ambao hawa hali zao zinaendelea vizuri.
Bumbuli amesema:“Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kikosi kipo tayari kwa mfano Mwamnyeto huyu amepona lakini mwalimu anahitaji kuona anapata muda wa kuwa fiti zaidi,”.