Home SPORTS BUMBULI: YANGA IPO IMARA KUNYAKUA POINTI TATU DHIDI YA GEITA.

BUMBULI: YANGA IPO IMARA KUNYAKUA POINTI TATU DHIDI YA GEITA.

Mwandishi wetu, DAR.

KIKOSI cha Yanga leo kinatua dimbani dhidi ya Geita Gold   katika mchezo utakaopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kikosi hicho kitawakosa baadhi ya wachezaji katika mchezo huo.

kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari , Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani lakini wapo tayari licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji.

Aliongeza kuwa Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki huyu alikuwa anatibu majeraha yake ila ameshapona na yupo tayari kwa mchezo ila atapumzishwa.

Pia Tonombe Mukoko ambaye ni kiungo huyu alikosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba pia aliwakosa Kagera Sugar na leo anakamilisha mchezo wake wa tatu kwa kuwa alikuwa na adhabu ya kadi nyekundu alionyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Simba katika Kombe la Shirikisho.

Pia wapo wale ambao wapo kwenye program maalumu ambao ni Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha pamoja na Dickson Ambundo ambao hawa hali zao zinaendelea vizuri.

Bumbuli amesema:“Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kikosi kipo tayari kwa mfano Mwamnyeto huyu amepona lakini mwalimu anahitaji kuona anapata muda wa kuwa fiti zaidi,”.

Previous articleSIMBA YAREJEA JIJINI DAR
Next articlePOLISI YAICHAPA AZAM FC 2-1
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here