Home BUSINESS NMB YATOA MISAADA YA MIL. 25/- KIGAMBONI

NMB YATOA MISAADA YA MIL. 25/- KIGAMBONI

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akionyeshwa mabenchi ya kukalia katika Hospitali ya Kigamboni na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard yaliyotolewa msaada na Benki hiyo.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Wilaya ya kigamboni, ikiwa ni pamoja na Mabenchi ya kukalia wagonjwa katika Hospitali ya Kigamboni, Madawati 50 kwa shule ya Msingi Ungindoni, Mabati 200 kwa Shule ya Msingi Rahaleo na Mabati 180 kwa Shule ya Sekondari Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 24 . Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni , Fatma Nyangasa akihutubia wakati wa kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Wilaya ya kigamboni, ikiwa ni pamoja na Mabenchi ya kukalia wagonjwa katika Hospitali ya Kigamboni, Madawati 50 kwa shule ya Msingi Ungindoni, Mabati 200 kwa Shule ya Msingi Rahaleo na Mabati 180 kwa Shule ya Sekondari Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 24. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akionyeshwa madawati na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Msingi Ungindoni.

Tamasha la Michezo baina ya timu za Wafanyakazi wa Benki ya NMB na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Bunge Sports Club’ likitambulika kwa jina la NMB Kivumbi na Jasho, limefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma na kufana.

Iilikuwa ni zaidi ya Kivumbi na Jasho, kuanzia katika matembezi ya taratibu yaliyoongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Phillip Isdor Mpango, hadi kwenye michezo saba iliyoshondaniwa, Kivumbi kikitimka zaidi katika mpira wa miguu na kikapu, ambako vuta nikuvute ilikuwa kubwa.

Katika mpira wa miguu, Bunge FC ilitoshana nguvu na NMB kwa dakika 90 ndani ya dimba la Jamhuri, ndipo Sheria ya upigaji penalti ulipotumika kumsaka bingwa, ambako Bunge FC waliibuka kidedea wakifunga penalti 4-3 katika mikwaju sita sita waliyopigiana.

Mnyukano kama huo ulikuwepo katika kikapu, ambako licha ya kutawala mechi na ‘kuupiga mwingi,’ NMB ilijikuta ikipoteza mcheza kwa kufungwa vikapu 70-57, hasira za kupoteza mchezo huo zikawapeleka katika riadha kwa hasira na kutawala mbio za mita 100 na 400 wanawake na wanaume.

Teddy George wa NMB akatwaa medali mbili za dhahabu mita 100 na 400 kwa wanawake akiwabwaga Rose Tweve na Queen Mlay wa Bunge, huku Nsolo Mlozi wa NMB naye akimgaragaza Aboubakar Assenga wa Bunge katika mita 100 wanaume, na kwenye mita 400 wanaume, Mlozi akitwaa medali akifuatiwa na Juma Kimori wa NMB pia.

Ushindi pekee wa Bunge katika mbio ni aliopata Naibu Spika, Tulia Ackson, aliyeshinda Mita 100 Menejimenti, akimshinda Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna aliyeshika nafasi ya pili akifuatiwa na Janeth Shango wa NMB pia katika nafasi ya tatu. 

Katika mbio za kukimbiza kuku, NMB iliibuka mabingwa upande wa wanawake na wanaume, ingawa ilifanya vibaya katika kuvuta kamba na wavu (wanawake na wanaume), ambako Bunge Sports Club ilishinda.

Previous articleRAIS SAMIA NI NYOTA INAYONG’AA
Next articleSIMBA QUEEN Vs LADY DOVES PATACHIMBIKA LEO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here