Home LOCAL RAIS SAMIA NI NYOTA INAYONG’AA

RAIS SAMIA NI NYOTA INAYONG’AA

Ukweli haujifichi, ilikuwa ni swala la muda tu Tanzania na Duniani kote kuona nyota kuu inayong’aa kwa Rais wetu kipenzi Mama wa Vitendo Samia Suluhu Hassan.

Leo umoja wa Machifu wamedhihirisha hilo katika tukio la kipekee sana huko Bujora Mwanza ambapo kwa pamoja umoja huo wa machifu wamempa Rais Samia jina la HANGAYA yaani nyota inayong’aa.

Hii ni siku chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kupitia Benki ya Dunia kuidhinisha kiasi cha takriban Dola za Marekani 567 kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kupambana na athari zilizotokana na UVIKO 19

Nyota ya Rais Samia inaangaza Afrika na Dunia nzima, Tarehe 04 mwezi huu Rais Samia alitajwa miongoni mwa wanawake bora Duniani kutoka Afrika wenye ushawishi mkubwa zaidi.

Chini ya uongozi wa *Chifu HANGAYA* Tanzania inaenda kuwa kilele cha utalii Afrika kupitia filamu ya Royal Tour ambayo Starling ni Rais mwenyewe, the Master-mind, Amiri Jeshi Mkuu, Mama wa Vitendo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania.

Nyota ya mama inafanya maajabu, Amani imetawala nchini, Miradi ya kimkakati inakwenda kwa kasi, wakulima wa cacao wanashangilia, ni fahari kuishi Tanzania.

Previous articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA AGFR
Next articleTCB YAZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here