NA: HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema Wafanyabiashara Wamachinga wa Manispaa ya Morogoro watagaiwa maeneo yao ya biashara bila kutoa rushwa.
Mkuu wa Wilaya Albert Msando alitoa taarifa hiyo leo katika mitandao ya kijamii akieleza kutekeleza agizo la Serikali kuwatengea maeneo ya Biashara Wamachinga wa Manispaa ya Morogoro.
“Katika Wilaya yangu natekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu, tutawagawia wafanyabiashara wetu maeneo kwa kufuata taratibu bila fujo ” alisema Msando.
Mkuu wa Wilaya Msando alisema wafanyabiashara wa Manispaa hiyo wa
Isalam, Mlapakolo ,Madaraka,Uhuru,na Luna watamia eneo la Soko Kuu Chifu Kingalu.
Taarifa hiyo ilisema wafanyabiashara watakaogaiwa eneo la biashara ni wamachinga walioandikwa majina na viongozi wao wa mitaa na walihakiki wenyewe majina yao kwa utaratibu huliowekwa .
Utaratibu wa kugawa maeneo ni wa WAZI. Mabanda yote yana namba,Ugawaji ni kutumia mfumo wa bahati nasibu. Utaokota namba kwenye pipa/box utaenda ilipo namba uliyookota.
Taarifa hiyo ilisema kuwa hakuna upendeleo zoezi hilo litasimamiwa na mkuu wa Wilaya mwenyewe hivyo wananchi wafanyabiashara wawe makini wasitapeliwe wala kutoa rushwa wote wana haki sawa .
HAKUNA yeyote atakayepewa nafasi kama hakuandikwa jina kwenye mtaa aliopo sasa na kila MTU atakikiwa jina lake .
Aidha Taarifa hiyo ilisema kuwa hakuna mfanyabiashara atakayepewa banda au meza ili amkodishie mtu mwingine na kumnyonya kodi pia alisema maeneo yasitengwa kwa biashara airusiwi kufanya biashara
Mwisho