Home LOCAL KEVELA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA UWIANO WA KIJINSIA KATIKA UTEUZI WA...

KEVELA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA UWIANO WA KIJINSIA KATIKA UTEUZI WA VIONGOZI

DAR ES SALAAM.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Mawaziri wapya watatu wakiwemo wanawake wawili hatua aliyodai imeendelea kuleta uwiano wa kijinsia katika uongozi nchini

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart alisema uteuzi wa Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kimeonyesha nia njema ya Rais Samia kuwaheshimisha wanawake.

Mbali na Mawaziri hayo Rais Samia pia alimteua Mbunge wa Bumbuli January Makamba kuwa Waziri wa Nishati na Madini akichukua nafasi ya Dk Medard Kalemani ambaye uteuzi wake pamoja aliyekuwa Waziri Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndugulile na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Dk Leonard Chamriho, ulitenguliwa.

“Kwa niaba ya wanawake wote wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe tunampongeza Rais Samia kwa uteuzi huu, na zaidi tunatambua jitihada zake za kuhakikisha wanawake wanashika nafasi muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu, nafasi ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikishikiliwa na wanaume”alisema Scolastika

Alisema uteuzi huo umeifanya Tanzania kutengeeneza historia kwa kuwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye ni mwanamke lakini pia mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kimsingi uteuzi huo umeongeza nafasi za wanawake mawaziri kufikia 7 sawa na asilimia 30.4 kutoka 5 sawa na asilimia 21.7 huku wanaume wakiwa ni 16 sawa na asilimia 69.6 jambo alilosema ni mwelekeo mzuri katika kufikia idadi ya hamsini kwa hamsini.

“Nitoe wito kwa viongozi wanawake na wanaume waliopo katika nafasi mbalimbali za uteuzi kutumia nafasi zao kikamilifu na kumsaidia Rais ili aweze kutimiza vyema majukumu yake ya kuleta maendeleo endelevu na jumuishi kwa Taifa letu” aliongeza Scolastika.

Alisema akiwa kama Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa Chama Mapinduzi Mkoa wa Njombe, kwa niaba ya wanawake wote wa Mkoa huo wanamuombe dua njema kwa Mungu ili aendelee kumpa Afya njema ya kuwaongoza watanzania.

Previous articleDC MSANDO WAMACHINGA WATAPA MAENEO BILA RUSHWA LEO
Next articleMHE. RAIS SAMIA, AZINDUA MKAKATI WA ELIMU YA UHAMASISHAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here