Home SPORTS AZAM KUKIPIGA LEO DHINI YA HORSEED

AZAM KUKIPIGA LEO DHINI YA HORSEED

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KIKOSI   cha Azam FC leo kitakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Horseed FC katika michuano ya  Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku katika  Uwanja wa Azam Complex.

Hata hivyo mchezo huo utachezwa  bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na maelekezo kutoka Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) ikiwa ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Azam FC imeweka wazi kuwa mashabiki na wadau wa soka wataweza kuushuhudia moja kwa moja mchezo huo wa leo Jumamosi dhidi ya Horseed, kupitia Azam TV chaneli ya Azam Sports HD 1 kuanzia saa 1.00 usiku.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema kuwa maandalizi ya mwisho yapo vizuri kwa kuwa kikosi kilishamaliza mazoezi na ni mchezo pekee unasubiriwa kwa sasa.

Pia kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 Azam FC iliweka kambi nchini Zambia na iliweza kucheza pia mechi za kirafiki.


Kipa wao namba moja Mathias Kigonya anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza leo.

Previous articleDIWANI BEATRICE AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU
Next articleRC MAKALLA AJITWISHA MGOGORO KATI YA WANANCHI NA MSITU WA PUGU KAZIMZUMBWI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here