Home SPORTS RC MAKALLA AJITWISHA MGOGORO KATI YA WANANCHI NA MSITU WA PUGU KAZIMZUMBWI.

RC MAKALLA AJITWISHA MGOGORO KATI YA WANANCHI NA MSITU WA PUGU KAZIMZUMBWI.

 

– Asema azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kutatua Migogoro ya Wananchi.

– Ataka Mgogoro huo kufika Mwisho.

– Awapa pole Wananchi kwa Mgogoro wao kudumu muda mrefu.

– Awataka TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu.

– Sasa kukutana na Wizara tatu za TAMISEMI, Mliasili na utalii na Wizara ya Ardhi kupata ufumbuzi.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Kufuatia Mgogoro wa Ardhi wa muda mrefu baina ya Wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu TFS juu ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameahidi kushughulikia Mgogoro huo kwa kushirikiana na Wizara tatu zinazohusika.

RC Makalla ametoa ahadi hiyo wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza Migogoro ya Wananchi ambapo Leo ni zamu ya Jimbo la Ukonga ambapo amesema azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kushughulikia Mgogoro ya Wananchi.

Miongoni mwa kilio Cha wananchi hao ni Matukio ya kupigwa, kuteswa na kukamatwa kwa Wakazi wanaozungukwa na Msitu huo ambapo RC Makalla amewaelekeza TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu na badala yake busara itumike.

Aidha RC Makalla amesema wakati anaendelea kushughulikia Mgogoro huo ni vyema TFS ikashirikiana na Wananchi hao na kupiga marufuku vitendo vya kukamata Wananchi wa Dar es salaam na kupeleka Wilaya ya Kisarawe.

Previous articleAZAM KUKIPIGA LEO DHINI YA HORSEED
Next articleMACHINGWA ARUSHA MJINI WAMLILIA GAMBO, ‘TUNAAMBIWA VITAMBULISHO VIMEZIKWA CHATO’
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here