Home LOCAL DIWANI BEATRICE AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU

DIWANI BEATRICE AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Mwalimu Beatrice Edward akiongea na wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bright African Leo September 11/2021 katika mahafali ya Darasa la saba(PICHA NA HERI SHAABAN).

Baadhi ya wanafunzi wa dsrasa la saba wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bright African Leo September 11/2021wakiwa katika mahafali ya Darasa la saba(PICHA NA HERI SHAABAN).

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Mwalimu Beatrice Edward akiwa na mwanafunzi wa darasa la awali wa Shule ya Msingi Bright African Leo September 11/2021 katika mahafali ya Darasa la saba(PICHA NA HERI SHAABAN)

NA: HERI SHAABAN (ILALA).

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala, Mwalimu Beatrice Edward amewataka wazazi na Walezi kuwekeza katika sekta ya Elimu kwa kuwajengea msingi bora watoto kwa ajili ya maisha ya baadae.

Diwani Beatrice alisema hayo Katika mahafali ya darasa la saba shule ya msingi BRIGHT AFRICAN ambayo yamefanyika Leo Kata ya Mzinga.

“Nawaomba wazazi na walezi kufatilia maendeleo ya watoto wetu katika sekta ya Elimu na kuwalea watoto katika misingi mema ili wawe na maadili waweze kufanya vizuri darasani na katika mitihani yao ya mkoa na ngazi ya Taifa” alisema Mwalimu Beatrice.

Diwani Beatrice alisema Taifa lolote ili liweze kupata maendeleo Wananchi wake lazima wasome na kupata elimu iliyo bora sio bora elimu.

Aidha Beatrice aliwataka Wazazi wa Wilaya ya Ilala  kuunga mkono juhudi za Serikali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu Sera ya elimu bira malipo kwa kuwasomesha watoto na kufatilia maendeleo yao kitaaluma.

Alisema Wanafunzi hawa ndio  madaktari wa kesho na Wabunge na mawaziri tuwalinde watoto wetu na kuwasomesha ili waweze kuwa na nidhamu.

Wakati huohuo amewataka Wanawake ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu kuchangamkia fursa za Serikali kwa  kukopa mikopo ya Serikali  ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ili wafanye biashara na Kupata fedha za kulipa ada kwa ajili ya elimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Kivule Amos Hangaya ameishauri Serikali kupunguza kodi za ada kwa Wamiliki wa Shule Binafsi ili waweze kuziendesha shule hizo na kuisaidia Serikali katika sekta ya elimu Tanzania ikuwe.

Mwenyekiti Amos Hangaya alisema ushauri huo aliotoa kwa Serikali waanze na Wilaya ya Ilala yaani Dar es Salaam baade ndio zifuate shule za mikoani wawashushie tozo.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya BRIGHT AFRICAN   Erneus Mgaya alisema  shule ya Bright African  ilianza 2012 ilisajiliwa mwaka 2016 mwaka huu ni mahafali ya NNE kwa darasa la saba.

Mwalimu Mgaya alisema shule ya  Bright African ina wanafunzi wa Chekechea hadi darasa la saba  ambapo shule ya awali wanafunzi 127 na shule ya Msingi wanafunzi 750  Walimu jumla 34.

Akielezea mafanikio ya elimu katika shule hiyo kitaaluma imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka katika mitihani ya darasa la NNE na darasa la saba ambapo alisema mwaka 2018 ilishika nafasi ya NNE kiwilaya  nafasi ya sita ngazi ya mkoa 192 ngazi ya Taifa   2019 nafasi ya sita Wilaya nafasi ya 40 ngazi ya Taifa.

Mwisho

Previous articleCAF YAZUIA MASHABIKI YANGA
Next articleAZAM KUKIPIGA LEO DHINI YA HORSEED
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here