Home LOCAL MHANDISI NA AFISA MANUNUZI WA HALMASHAURI YA BUNDA, MIKONONI MWA TAKUKURU

MHANDISI NA AFISA MANUNUZI WA HALMASHAURI YA BUNDA, MIKONONI MWA TAKUKURU

Na: Mwandishi Wetu, BUNDA.

ZIARA ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, RC Ally Hapi, Leo imeingia kwenye Halmashauri ya Bunda na imeahirishwa mpaka kesho huku ikiacha imewaweka mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) watumishi wawili wa Halmashauri hiyo.

Walioondoka na TAKUKURU baada ya ukaguzi wa Miradi mitano ya maendeleo ni Mhandisi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Raulent Marashi na Afisa Manunuzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Mboji.

Hatua hiyo imefuatia miradi yote hiyo kukutwa na mapungufu mengi, ambayo kwa hatua za awali yameonekana kusababishwa na miradi kutosimamiwa vizuri, uzembe, matumizi mabaya ya fedha na kukosekana uadilifu.

Kwamfano Mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri hiyo, uliopo Kibara Jimbo la Mwibara licha ya Serikali kupeleka Sh bilioni Moja ili utekelezaji uanze Machi Mwaka huu, mpama sasa ndiyo wanachimba msingi.

RC Hapi amesema hata utaratibu wa ununuzi umekiukwa, vifaa vilivyokutwa eneo la mradi ikiwemo Nondo, Mbao, Miti aina ya Milunda, imeelezwa kuwa vilinunuliwa kwa mawakala kinyume na miongozo inayotolewa na serikali.

Alipohojiwa kwanini hawakununua simenti na nondo viwandani, Mboji amesema kitengo chake kinakabiliwa na upungufu wa watumishi.

Naye Mhandisi Marashi alipohojiwa sababu za mradi huo kuchelewa amesema hana sababu.

Kwa mujibu wa Mhandisi Marashi walipewa muda wa miezi Sita kukamilisha mradi hivyo umebaki mwezi Mmoja, muda ambao hautoshi kufikia malengo.

Pamoja na maagizo mengine, RC amemtaka Afisa wa TAKUKURU wa Wilaya hiyo,Mohamed Paul kuanza kazi yake usiku huu wa Agost 15 na kuondoka inakojengwa  Hospitali ya Wilaya na watumishi hao kwa ajili ya mahojiano.

Ametaka kesho asubuhi apewe taarifa ya awali ili hatua zaidi zichukuliwe kwa lengo la kukwamua miradi hiyo na kuwaletea wananchi maendeleo kama ambavyo inaelekezwa na Rais, Samia Suluhu Hassan.

Previous articleACT WAZALENDO WATUMA SALAMU KWA RAIS MTEULE ZAMBIA.
Next articleWAZIRI MKUU ATANGAZA ZABIBU KUINGIZWA KWENYE MAZAO YA KIMKAKATI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here