Home LOCAL ACT WAZALENDO WATUMA SALAMU KWA RAIS MTEULE ZAMBIA.

ACT WAZALENDO WATUMA SALAMU KWA RAIS MTEULE ZAMBIA.

DAR ES SALAAM.

Chama cha ACT Wazalendo  kimemtumia Salaam za pongezi Rais Mteule wa Zambia, Ndg. Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Zambia.

Taarifa ya Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya chama hicho leo Agosti 15,2021 imesema kwa kuzingatia matokeo rasmi yaliyokwishatangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) na baada ya Rais Edgar Lungu kukiri kushindwa ni dhahiri kuwa Ndugu Hakainde Hichilema ambaye ni mgombea wa chama cha upinzani cha UPND amevuka wigo wa zaidi ya asilimia 50 (50%+1) ya kura zote.

Taarifa hiyo ya ACT Wazalendo iliyosainiwa na Mkuu wa  Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fatma Abdulhabib Ferej imesema kwa matokeo hayo, Hakainde  Hichilema ameshinda uchaguzi huo mkuu na kumuacha mbali mgombea aliyekuwa akitetea nafasi hiyo ya Urais, Ndugu Edgar Chagwa Lungu. 

“Sisi ACT Wazalendo tukiwa ni Chama kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania na Chama rafiki wa Chama cha UPND, tunampongeza Ndugu Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa saba wa Jamhuri ya Zambia.

“Ni matumaini yetu kuwa, chini ya uongozi wa Hakainde Hichilema, nchi zetu mbili- Tanzania na Zambia, zitashamirisha na kuimarisha uhusiano wa kihistoria katika nyanja za kiuchumi, miundombinu na kikanda kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).” Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha ACT Wazalendo kimemtakia mafanikio Rais huyo mpya katika majukumu yake mapya ya kuitumikia Zambia na hivyo kutimiza matakwa ya wananchi wa nchi hiyo. 

Mwisho

Previous articleKISWAHILI CHATENGEWA RASMI BAJETI YAKE SADC,SUALA LA KATIBU MTENDAJI MPYA LAACHWA MIKONONI MWA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI
Next articleMHANDISI NA AFISA MANUNUZI WA HALMASHAURI YA BUNDA, MIKONONI MWA TAKUKURU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here