Home BUSINESS KACU KUANZA KUUZA MAROBOTA YA PAMBA ULAYA

KACU KUANZA KUUZA MAROBOTA YA PAMBA ULAYA

Abduly Ally Kaimu Meneja ja wa Kiwanda kinachomilikiwa na Chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) akitoa ufafanuzi.

Marobota ya Pamba yaliofungwa tayari kwa kuuzwa njee ya Nchi
 

Na: Saimon Mghendi, KAHAMA.

CHAMA kikuu cha Ushirika KACU kimesema kuwa kulingana na ubora wa Pamba inayochakatwa na kiwanda cha kuchambua Pamba kilichopo Kata ya Mhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Ushirika huo umeanza kufanya biashara ya zao hilo na mataifa ya Ulaya jambo ambalo limesababisha zao hilo kuonekana kuwa na tija nchini.

Kaimu Meneja Mkuu wa chama hicho Abdul Ally amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea kiwanda hicho.

Kaimu Meneja huyo amesema kuwa lengo la KACU  kwa msimu huu wa zao la Pamba ni kununua kilo Milioni 6 kutoka kwa wakulima wa zao hilo wa halmashauri za Ushetu, Kahama, Msalala, Nyang’hwale, Kishapu na Meatu.

Kwa upande mwingine kiongozi huyo amesema kuwa chama chake cha ushirika kimejipanga kuanzisha kiwanda kingine cha kusindika mafuta ya kula ili kuongeza ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo na shinyanga kwa ujumla.

Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya watumishi wa kiwanda hicho wamepongeza uongozi wa chama hicho cha ushirika kwa kuwapa vijana fursa za ajira wanaozagaa mitaani jambo linalopelekea kutunza familia zao na kuachana na vitendo viovu.

MWISHO.


Previous articleBYABATO: ATAKAYEKWAMISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI HATAACHWA SALAMA.
Next articleCRDB BANK INTERNATION MARATHON 2021 YAFANIKIWA KUKUSANYA NUSU BILIONI KUSAIDIA AFYA NA MAZINGIRA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here