Home SPORTS CRDB BANK INTERNATION MARATHON 2021 YAFANIKIWA KUKUSANYA NUSU BILIONI KUSAIDIA AFYA NA...

CRDB BANK INTERNATION MARATHON 2021 YAFANIKIWA KUKUSANYA NUSU BILIONI KUSAIDIA AFYA NA MAZINGIRA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akishiriki mbio za CRDB Internation Marathon 2021 Km. 5 zilizofanyika leo jijini Dar es salaam akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel,Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongollo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Amos Makallana kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela.


Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni Benki ya CRDB Bi. TullyEsther Mwambapa akishiriki katika mbio hizo zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya washiriki mbalimbali wa mbio hizo wakishiriki katika barabara mbalimbali ambazo zilipitia.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akishiriki mbio za CRDB Internation Marathon 2021 Km. 5 zilizofanyika leo jijini Dar es salaam akiwa katika mazoezi ya kupasha mwili na viongozi mbalimbali mara baada ya kukimbia mbio za Km.5 katika mbio za CRDB Marathon 2021.

Washiriki wa mbio hizo kutoka makampuni mbalimbali wakishiriki katika mazoezi maalum ya kupasha mwili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Ally Laay pamoja na viongozi mbaimbali wakishiriki katika mazoezi.

Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB wakishiriki katika mazoezi mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.


Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB wakishiriki katika mazoezi mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.


Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni Benki ya CRDB Bi. TullyEsther Mwambapa akizungumza wakati akikaribisha viongozi mbalimbali na washiriki wa mbio hizo zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni Benki ya CRDB Bi. TullyEsther Mwambapa akizungumza wakati akikaribisha viongozi mbalimbali na washiriki wa mbio hizo zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza mara baada ya kushiriki mbio hizo.

Mbio za hisani za kimataifa zilizoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank International Marathon” kwa mwaka 2021 zimefanikiwa kuandika rekodi kwa kuvutia washiriki zaidi ya 5,000 ikiwamo maelfu ya raia wa kigeni.

Jumla ya Shilingi za Kitazania Shilingi milioni 500 zimefanikiwa kukusanywa ambazo zitaelekezwa kwa ajili ya kusaidia jamii.

Akizungumza na washiriki, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio hizo, aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Benki ya CRDB kwa kufanikisha mbio hizo zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo JKCI, kujenga kituo cha mawasiliano cha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kusaidia utunzaji mazingira kupitia kampeni ya Pendezesha Tanzania.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali inasikia fahari kuona taasisi za kizalendo kama Benki ya CRDB zikiwa mstari wa mbele katika kusaidia Serikali kuboresha sekta za kijamii kama vile; afya, elimu na mazingira na huku akikiri kwa dhati kuwa mbizo hizo zinazofanyika kila mwaka kuwa ni fursa adhimu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwekeza katika ustawi wa jamii.

“Nimekuja hapa kwa lengo la kuonyesha kuwa Serikali inaunga mkono na kufurahishwa sana na ubunifu huu wa Benki ya CRDB. Kwa niaba ya Serikali niwashukuru kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kwa kuboresha huduma za afya kwa umma,” ameeleza Waziri Mkuu.

Aliwapa kongole viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwamo; Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel na washiriki wengine wote kwa kuunga mkono jitihada hizo ambazo zimejielekeza katika kuokoa maisha ya wale wenye uhitaji katika jamii na kuboresha mazingira.

“Nafahamu wazi kuwa ni ngumu miongoni mwenu kuamka asubuhi sana hususan katika hali hii ya hewa ya baridi na siku za mapumziko, lakini mmeweza kuzishinda nafsi zenu na kuacha shuka zenu pembeni ili kuja kushiriki katika mbio hizi,” aliongezea.

Alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kuendelea kusaidia upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo. Waziri Mkuu alisema uamuzi huo utaendelea kusaidia kupunguza makali ya gharama kwa ajili ya upasuaji wa moyo ambazo watu wengi hawawezi kuzimudu pamoja na Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 80.

“Wazo hili la kuendelea kusaidia gharama za upasuaji kwa watoto ni uamuzi mzuri sana kwani hata asilimia 20 iliyobaki wazazi wengi hawana uwezo wa kuchangia. Hongereni kwa kurejesha tabasamu kwa watoto na kuwapatia tumaini la maisha,” Waziri Majaliwa alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alibainisha kuwa mbizo za mwaka huu zimevuka lengo la ukusanyaji wa Shilingi milioni 500, akitoa shukrani kwa makampuni na taasisi zilizojitokeza kushirikiana na benki hiyo pamoja na wakimbiaji waliojitokeza kutoka ndani na nje ya nchi.

“Kati ya fedha zote Shilingi Milioni 500 zilizopatikana katika mbio hizo, Shilingi Milioni 200 zimeelekezwa JKCI, Sh104 milioni zimeenda ORCI na kiasi kilichobaki kimeelekezwa katika kampeni za utunzaji wa mazingira,” alisema Nsekela.

Nsekela aliwashukuru Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof, Mohammed Janabi na Mkurugenzi Mkuu wa ORCI, Dkt. Julius Mwaiselage kwa ushirikiano wao huku akiweka mkazo kuwa kauli mbiu ya benki hiyo isemayo “Kasi Isambazayo Tabasamu” imefanikiwa kutokana na mchango wao wa dhati.

Katika maelezo yake ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa alisema asilimia 85 ya washiriki wa mbio hizo ni Watanzania huku akibainisha kuwa wakimbiaji wa kimataifa waliojisali kutoka nje ya Tanzania ni zaidi ya 700.

Akiongezea, Tully alisema mbio hizo za CRDB Bank International Marathon ambazo zimeendelea kutambulika kimataifa baada ya kupatiwa ithibati na World Athletics na AMIS, kwa sasa zina hadhi sawa na zile mbio za Sanlam Cape Town Marathon za Afrika Kusini na Boston Marathon za nchini Marekani.

“Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa mbio hizi za CRDB zinarejesha heshima ya Tanzania ya michezo katika taswira ya dunia,” anaeleza Tully. Huku zaidi ya wakimbiaji wa kimataifa 700 wakishiriki katika mbio za mwaka huu.

Mbio hizo zimeendelea kupata mwamko mkubwa kutoka kwa wakimbiaji kutokana na lengo lake la kusaidia kusaidia jamii. Hii ni mara ya pili Benki ya CRDB inaandaa mbio hizi kwa mafanikio makubwa, baada ya zile zilizofanyika mwaka na kukusanya Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya upasuaji wa watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Mbio za mwaka jana zilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu ambaye kwa wakati huo alikuwa akihudumu kama Makamu wa Rais.Katika matokeo ya mbio hizo, Paulo Ayanaye raia wa Kenya aliibuka kinara wa mbio za 42km kwa upande wa wanaume akitumi muda wa 02:15:28, wakati Shelmith Nyawira raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wa wanawake akitumia muda wa.

Kwa mbio za 21km, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Mkungo Panuel raia wa Kenya akitumia muda wa 01:03:19, kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Pauline Esikon raia wa Kenya baada ya kutumia muda wa 01:12:17.

Katika mbio za 10km, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Joseph Tiophil raia wa Tanzania alitumia muda wa 00:28:51, kwa wanawake Transfora Musa raia wa Tanzania ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 00:33:52.

Katika mashindano ya mbio za baiskeli 65km, Masunga Duba raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume baada ya kutumia muda wa 01:49:07, upande wa wanawake Swabra Abdallah raia wa Tanzania ameibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 02:06:39.

Washindi 32 katika mbio hizo wamejizolea jumla ya Shilingi Milioni 50.

 

Previous articleKACU KUANZA KUUZA MAROBOTA YA PAMBA ULAYA
Next articleKISWAHILI CHATENGEWA RASMI BAJETI YAKE SADC,SUALA LA KATIBU MTENDAJI MPYA LAACHWA MIKONONI MWA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here