Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza (wa pili kulia) akifafanua Jambo mbele ya wajasiriamali wanachama wa TWCC walipofanya ziara fupi ya kupita kwenye mabanda ya wajasiriamali hao kujionea namna wanavyofanya shughuli zao. ( Wakwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akiweka saini kwenye kitabu maalum katika Ofisi ya TWCC iliyopo ndani ya Banda lao mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuzungumza na wajasiriamali wao kwenye mabanda yao. (PICHA NA: HUGHES DUGILO) |
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC) kimewapongeza wajasiriamali na wafanyabiashara waliojitokeza kushiriki maonesho ya 45 ya kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi kwenye mahojiano maalum na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla amesema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuweza kutangaza Biashara zao na kutengeneza mtandao wa kibiashara baina yao na wadau wengine wanaofika kutembelea maonesho hayo.
Ameongeza kuwa mara zote wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa za kibiashara pindi zinapojitokeza na wao kama viongozi wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanawasaidia kufanya shughuli zao bila vikwazo vyovyote huku akiipongeza Serikali chini ya Rais Mama Samia Hassan Suluhu kwa uongozi wake madhubuti.
‘’kama mnavyoona ndugu zangu waandishi wa habari hapa tupo sabasaba kuna wanawake kutoka mikoa yote Tanzania ikiwemo visiwani Zanzibar na wamekuja na bidhaa mbalimbali ambazo wanatengeneza kwa mikono yao wenyewe hivyo sisi kama Twcc tunawasaidia na kuwapa fursa hizi mbalimbali ili kuweza kutangaza bidhaa zao na kuweza kutambulika zaidi kimataifa .”alisema Mwenyekiti Mercy.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Twcc amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa na muamko mkubwa na mamlaka husika wamejitahdi kufanya maandalizi mazuri na watu wengi wamekuwa wakitembelea maonesho hayo ikiwa ni siku chache tu toka kufunguliwa na kuwataka wananchi hususani wakazi wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani kufika kwenye Banda lao.
“Tunawakaribisha watu ambao wanataka kuwekeza na wanawake kwani kuina vitu vizuri hivyo waje kushirikiana katika biashara na kitu chatofauti ambacho wanaweza kukipata vipo vingi mno kikubwa waje kwa wingi hapa “