Home BUSINESS JATU PLC YATUA SABASABA KWA KISHINDO, WANANCHI WAMIMIKA KUPATA HUDUMA ZAO.

JATU PLC YATUA SABASABA KWA KISHINDO, WANANCHI WAMIMIKA KUPATA HUDUMA ZAO.


Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
WATANZANI wameshauriwa kujitokeza kwenye viwanja vya maonyesho sabasaba wilayani Temeke ili kuona fursa mbalimbali ambazo zinapatikana kupitia maonyesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda  Profesa Kitila Mkumbo.

Rai hiyo imetolewa Wilayani humo na Ngorosho Winfrid  ambaye ni Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Jatu PLC ambapo alisema kuna haja ya Wananchi kutembelea maonyesho hayo ili kuona fursa zilizomo.

Amesema wao kama Jatu PLC wapo kwenye viwanja hivyo vya kimataifa vya Mwalimu Nyerere maalufu kama Sabasaba Kwa ajili ya kuwapa fursa ya kununua hisa watanzania na kuwa sehemu ya kampuni hiyo.

“Sisi kama Jatu tupo kwenye viwanja hivi vya Mwalimu Nyerere Sabasaba na kubwa zaidi tumekuja na kauli mbiu yetu ya Buku tano inatosha ambapo fedha hiyo itamwezesha mwananchi kununua Hisa.” Amesema Ngorosho

Nakuongeza kuwa “ili kuweza kupata fursa ya kupata hisa Jatu inakiwa kufika kwenye Banda lao ukiwa na kitambulisho cha NIDA na shilingi 5000 mkononi itakufanya kununua hisa ambapo hisa moja ni shilingi mia 500.

Amefafanua kuwa wapo katika hatua za mwisho kwani kampeni hiyo ya buku tano inatosha inatamatika mwezi julai Mwaka huu hivyo nivema kama Wananchi wangechangamka katika siku hizi zilizobakia.

Ngorosho ambaye ni Afisa Masoko aliongeza kuwa Jatu PLC nikampuni ya kitanzania ambayo mwanzilishi wake ni mtanzania na amedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo.

Amesema Jatu licha ya mambo ya hisa lakini imejikita kwenye kilimo ambapo wanafanya kilimo karibu maeneo mbalimbali hapa nchini lakini sio kilimo tu hadi masoko wanayo ndani na nje ya nchi.
Previous articleKUTANA NA MJASIRIAMALI ANAETENGEZA SABUNI YA MAZIWA YA MBUZI.
Next articleTWCC YAANZA KWA KISHINDO MAONESHO YA SABASABA, YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here