Warembo wakiwakaribisha wageni mbalimbali wanaofika kwenye Banda la Shirika la Madini la Taifa STAMICO katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. |
NA: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kuwa lipo kwenye maandalizi ya kutengeneza mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya makaa ya mawe ili uweze kutumika katika matumizi ya majumbani na kusaidia kuwapunguzia gharama wananchi na kusaidia kutunza mazinga.
hayo yamesemwa na Mhandisi Mtaalam wa Uchenjuaji Madini kutoka Shirika hilo Mhandisi Happy Mbenyange alipokuwa akimueleza katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Zanzibar Mhe. Juma Reli alipofanya ziara fupi ya kutembelea Banda la STAMICO lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Madini kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa tayari wameshafanya majaribio lengo likiwa kuwafanya wananchi kuacha kutumia mkaa wa miti na kutunza Mazingira.
Amesema kuwa mkaa huo ni rafiki na kwamba tayari kuna mtambo maalum ambao umeagizwa utakaoweza kutengeneza mkaa huo katika umbo la duara hivyo mara baada ya kuwasili kwa mtambo huo shughuli rasmi za uzalishaji zitaanza tayari kwaajili ya kuusambaza kwa wananchi kwa kutumia mawakala mbalimbali kwenye mikoa yote Nchini.
“STAMICO kwa kuunga juhudi za Serikali za kutunza mazingira tumekuja na products mpa huu ni mkaa unaotumika kupikia majumbani kwahiyo tunachimba mkaa wetu tunaupunguza nguvu na kuweza kutumika nyumbani, haauna moshi, hauna majivu na sumu zote zimetolewa kwaajili ya matumizi ya nyumbani” Amesema Mhandisi Happy.
Ameongeza kuwa Mgodi wa Kiwira una makaa ya kutosha hivyo wataweza kuzalisha Bidhaa hiyo kwa muda mrefu na kutosheleza kwa matumizi ya muda mrefu na kwamba watanzania wajiandae kuipokea Bidhaa hiyo.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa STAMICO Bibiana Ndumbaro amesema kuwa wao kama Shirika wamefika kwenye maonesho ya sabasaba mwaka huu wakiwa na vitu vingi vya kuwaelimisha wananchi hivyo kuwaomba wananchi wote hususani wakazi wa Dar es Salaam kufika kwenye Banda lao ili kuweza kupata Elimu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo ikiwemo Bidhaa mpya ya mkaa mbadala utakaozalishwa kutokana na mabaki ya makaa ya mawe kutoka kiwira.
“Ombi langu kwa wananchi ni kuweza kufika kwenye maoesho haya na kutembelea Banda letu kwani watapata fursa ya kufahamu na kujifunza mambo mengi na kuweza kujua namna ambavyo Shirika linatekeleza majukumu yake” Amesema Bibiana.
Maonesho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 5 mwaka huu na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kufungwa tarehe 13 Julai,2021.