Home BUSINESS STAMICO YAJA NA BIDHAA MPYA YA MKAA WA MAJUMBANI UNAOTOKANA NA MABAKI...

STAMICO YAJA NA BIDHAA MPYA YA MKAA WA MAJUMBANI UNAOTOKANA NA MABAKI YA MAKAA YA MAWE.

Mwandisi mchenjuaji Madini wa Shirika la Madini la Taifa Happy Mbenyange (wa pili kushoto) akitoa maelezo jinsi ambavyo Shirika hilo lilivyojiandaa kutengeneza mkaa ambao utatuma majumbani kupikia kutoka katika makaa ya mawe ya kiwira kwa katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Zanzibar Mhe. Juma Reli (wa pili kulia) alipofika kwenye Banda la STAMICO lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kushoto) ni Afisa Uhusiano wa STAMICO Bibiana Ndumbaro.

katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Zanzibar Mhe. Juma Reli (kulia) akitia saini Kitabu cha wagaeni mara Baada ya kumaliza ziara yake fupi ya kutembelea Banda la STAMICO kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Warembo wakiwakaribisha wageni mbalimbali wanaofika kwenye Banda la Shirika la Madini la Taifa STAMICO katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Fundi Sanifu Madini  kutoka STAMICO Ignas Mchira (kushoto) akitoa elimu kwa moja ya wageni waliofika kwenye Banda la Shirika hilo kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Mjiolojia wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Revocatus  Mafungo (wa kwanza kushoto) akitoa Elimu ya namna ambavyo Shirika hilo linavyofanya Shughuli zake kwa wananchi waliotembelea kwenye Banda lao katika Maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bibiana Ndumbaro (kushoto) akifafanua jambo alipokuwa kwenye mahojiano maalum kwenye Banda lao katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.  (kulia) ni Afisa wa Shirika hilo Marc Nahungo.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bibiana Ndumbaro (aliyekaa) akiwa na Maofisa wa Shirika hilo Mhandisi Happy Mbenyange (kushoto) na Bilton Otto (kulia waliosimama) kwenye Picha ya pamoja ndani ya Banda lao.

Mamisi waliopo ndani ya Banda la STAMICO ni warembo ambao wapo maalum kwa ajili ya kutangaza na  kutoa elimu kuhusu mkaa mbadala wa Makaa ya mawe Rafiki briquette.(wa kwanza kusho) ni Hellen Chepe, (wa pili kushoto) ni Subilaga Ambangile, (wa tatu kushoto) ni Miriam Belinda, na (wa kwanza kulia) ni Anna Frank. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).  

NA: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kuwa lipo kwenye maandalizi ya kutengeneza mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya makaa ya mawe ili uweze kutumika katika matumizi ya majumbani na kusaidia kuwapunguzia gharama wananchi na kusaidia kutunza mazinga.

hayo yamesemwa na Mhandisi Mtaalam wa Uchenjuaji Madini kutoka Shirika hilo Mhandisi Happy Mbenyange alipokuwa akimueleza katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Zanzibar Mhe. Juma Reli alipofanya ziara fupi ya kutembelea Banda la STAMICO lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Madini kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa tayari wameshafanya majaribio lengo likiwa kuwafanya wananchi kuacha kutumia mkaa wa miti na kutunza Mazingira.

Amesema kuwa mkaa huo ni rafiki na kwamba tayari kuna mtambo maalum ambao umeagizwa utakaoweza kutengeneza mkaa huo katika umbo la duara hivyo mara baada ya kuwasili kwa mtambo huo shughuli rasmi za uzalishaji zitaanza tayari kwaajili ya kuusambaza kwa wananchi kwa kutumia mawakala mbalimbali kwenye mikoa yote Nchini.

“STAMICO kwa kuunga juhudi za Serikali za kutunza mazingira tumekuja na products mpa huu ni mkaa unaotumika kupikia majumbani kwahiyo tunachimba mkaa wetu tunaupunguza nguvu na kuweza kutumika nyumbani, haauna moshi, hauna majivu na sumu zote zimetolewa kwaajili ya matumizi ya nyumbani” Amesema Mhandisi Happy.

Ameongeza kuwa Mgodi wa Kiwira una makaa ya kutosha hivyo wataweza kuzalisha Bidhaa hiyo kwa muda mrefu na kutosheleza kwa matumizi ya muda mrefu na kwamba watanzania wajiandae kuipokea Bidhaa hiyo.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa STAMICO Bibiana Ndumbaro amesema kuwa wao kama Shirika wamefika kwenye maonesho ya sabasaba mwaka huu wakiwa na vitu vingi vya kuwaelimisha wananchi hivyo  kuwaomba wananchi wote hususani wakazi wa Dar es Salaam kufika kwenye Banda lao ili kuweza kupata Elimu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo ikiwemo Bidhaa mpya ya mkaa mbadala utakaozalishwa kutokana na mabaki ya makaa ya mawe kutoka kiwira.

“Ombi langu kwa wananchi ni kuweza kufika kwenye maoesho haya na kutembelea Banda letu kwani watapata fursa ya kufahamu na kujifunza mambo mengi na kuweza kujua namna ambavyo Shirika linatekeleza majukumu yake” Amesema Bibiana.

Maonesho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 5 mwaka huu na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kufungwa tarehe 13 Julai,2021.


Previous articleMHE. RAIS SAMIA ASHUHUDIA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA DIMBA LA MKAPA DAR.
Next articleWANANCHI WAENDELEA KUMIMIKA BANDA LA BRELA KUPATA USAJILI WA BIASHARA MAONESHO YA SABASABA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here