Home BUSINESS WANANCHI WAENDELEA KUMIMIKA BANDA LA BRELA KUPATA USAJILI WA BIASHARA MAONESHO YA...

WANANCHI WAENDELEA KUMIMIKA BANDA LA BRELA KUPATA USAJILI WA BIASHARA MAONESHO YA SABASABA.

Watu mbalimbali ambao wamefika kwenye Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kupata huduma katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ambapo BRELA imeshiriki maonesho hayo na kutoa huduma zake ikiwemo na kutoa vyeti Papo kwa hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma BRELA Rhoida Andusamile (wa pili kulia) akiwa na Afisa TEHAMA Joram Manyika (kushoto) wakizungumza na mteja aliyefika kwenye Banda lao kupata huduma katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yajulikanayo kama Sabasaba.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma BRELA Rhoida Andusamile (kulia) akijadiliana jambo na Afisa TEHAMA Manyika (kushoto) wakiwa kwenye Banda lao kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Afisa TEHAMA  Hillary Mwenda (aliyesimama) akimkabidhi karatasi yenye taarifa muhimu mteja aliyefika kwenye Banda hilo kwaajili ya kupata huduma.
Maofisa wa BRELA wakitoa huduma za usajili wa Biashara na Leseni kwenye maonesho hayo. (wa kwanza kushoto) ni Frank Filimbi, (katikati) ni Rehema Kionaumela, na (kulia) ni Angela Kimaro  
Afisa TEHAMA Mwenda akipitia taarifa mbalimbali za wateja waliokwisha pata huduma kwenye maonesho hayo
Afisa BRELA Swedi Gabriel (aliyevaa fulana nyeusi) akiwapokea wananchi waliojitokeza kwenye Banda lao kwaajili ya kupata maelezo mbalimbali yanayohusu BRELA.

Muonekano wa Banda la BRELA lililopo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. (PICHA: NA: HUGHES DUGILO).

Previous articleSTAMICO YAJA NA BIDHAA MPYA YA MKAA WA MAJUMBANI UNAOTOKANA NA MABAKI YA MAKAA YA MAWE.
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.PILI JULAI 4-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here