Home BUSINESS KUTANA NA MJASIRIAMALI ANAETENGEZA SABUNI YA MAZIWA YA MBUZI.

KUTANA NA MJASIRIAMALI ANAETENGEZA SABUNI YA MAZIWA YA MBUZI.

DAR ES SALAAM.

MENEJA Mauzo kutoka Kampuni ya GCAT  ambao ni wazalishaji wa bidhaa za afya na vipodozi salama Mariam Matoloka ametoa rai kwa watanzania kupenda kutumia bidhaa za kiasili ili kuweza kuboresha ngozi ya mwili.

Amesema kuwa bidhaa za kiasili zinafanya mwili kuwa safi na salama sana Kwa ngozi ya mwili hivyo nivema Wananchi wakajenga mazoea ya kutumia bidhaa asilia.

Akizungumza kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam barabara ya Mariam amewaomba wananchi kutembelea kwenye maonyesho hayo nawafika kwenye Banda la Tabwa ili kupata bidhaa hizo.

“Hapa tuna sabuni za maziwa ya mbuzi ambazo zinafanya ngozi ya mwili kuwa safi na salama lakini pia zinaondoa mikunjo katika mwili ,zinakuweka mwili kuwa nyororo .hivyo waje watumie Sabasaba hii kupata bidhaa bora kabisa.” Amesema.

Amefafanua kuwa licha ya uwepo wao kwenye viwanja hivyo vya sabasaba lakini pia ofisi zao zipo Masaki jijini Dar Es Salaam na mbagala Wilayani temeke lakini pia wanapatikana Kariakoo, kinondoni ,tegeta.
Ameongeza kuwa Bidhaa yao hiyo ya Sabuni ni nzuri kwani iweza kurudisha ngozi kwenye uasili wake kama imeungua na jua .inasaidia hata watoto ,inaondoa mapunye mba, na mambo mengine mbalimbali katika mwili hivyo wajitokeze kupata huduma hizo.
Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 1-2021
Next articleJATU PLC YATUA SABASABA KWA KISHINDO, WANANCHI WAMIMIKA KUPATA HUDUMA ZAO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here