NA: HERI SHAABAN- IRINGA.
MKUU wa Mkoa IRINGA Quine Sendiga anatarajia kuzindua usafi katika Manispaa hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Kampeni ya Usafi .
Kampeni hiyo inatarajia kuzinduliwa Juni 26 mwaka huu katika Manispaa hiyo ambapo vikundi mbalimbali vinatarajia kushiriki katika usafi huo.
Akizungumza katika Kampeni hiyo Afisa Mazingira wa Manispaa IRINGA Ardom Mapunda alisema Kampeni hiyo ya IRINGA SAFI CAMPAIGN itakuwa pia kuna matembezi Maalum ya hiyari kwa ajili ya kuhamasisha siku hiyo na kutoa elimu.
“Mkuu wa Mkoa anatarajia kuzindua usafi katika Manispaa yetu kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu kutekeleza agizo la usafi kwani ni usafi ni afya” alisema Mapunda.
Mapunda Alisema’ usafi ni jukumu letu siku hiyo kutoa elimu kwa wananchi sambamba uzinduzi.
Alisema lengo la kampeni ya usafi wa Manispaa ya Iringa, i kuhamasisha wananchi kufanya usafi na kuhifadhi mazingira na kuendeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa Jumamosi na kuunga mkono juhudi za Mh. Rais mama yetu Samia Suluhu Hassani
Aidha alisema Kampeni hiyo uzinduzi wake vikundi mbalinbali Vitapamba siku hiyo Jumuiya za usafi , asasi za kiraia, Skauti na wananchi watashiriki.
Aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuwa wasafi ili Manispaa Iringa iwe safi kila wakati kwani usafi inawezekana.
Mwisho