Home LOCAL RC SENDIGA KUZINDUA USAFI MANISPAA YA IRINGA

RC SENDIGA KUZINDUA USAFI MANISPAA YA IRINGA

NA: HERI SHAABAN- IRINGA.

MKUU wa Mkoa IRINGA  Quine Sendiga anatarajia kuzindua usafi katika Manispaa hiyo  kwa ajili ya kuunga mkono Kampeni ya Usafi .

Kampeni hiyo inatarajia kuzinduliwa Juni 26 mwaka huu katika Manispaa hiyo ambapo vikundi mbalimbali vinatarajia kushiriki katika usafi huo.

Akizungumza katika Kampeni hiyo Afisa Mazingira wa Manispaa IRINGA Ardom Mapunda alisema Kampeni hiyo ya IRINGA SAFI CAMPAIGN  itakuwa pia kuna matembezi Maalum ya hiyari kwa ajili ya kuhamasisha siku hiyo na kutoa elimu.

“Mkuu wa Mkoa anatarajia kuzindua usafi katika Manispaa yetu kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu kutekeleza agizo la usafi kwani ni usafi ni afya” alisema Mapunda.

Mapunda Alisema’ usafi ni jukumu letu siku hiyo  kutoa elimu kwa wananchi sambamba uzinduzi.

Alisema lengo la  kampeni ya usafi wa Manispaa ya Iringa, i kuhamasisha wananchi kufanya usafi na kuhifadhi mazingira na  kuendeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa Jumamosi na kuunga mkono juhudi za Mh. Rais mama yetu Samia Suluhu Hassani 

Aidha alisema Kampeni hiyo uzinduzi wake vikundi mbalinbali Vitapamba siku hiyo  Jumuiya za usafi , asasi za kiraia, Skauti na wananchi watashiriki.

Aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuwa wasafi ili Manispaa Iringa iwe safi kila wakati kwani usafi inawezekana.

Mwisho

Previous articleCLOCK TOWER MARATHON YAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA SASA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 8 MWAKA HUU, MEYA ASEMA YATAFUFUA UTALII.
Next articleWANAWAKE WATAKIWA KUWA MAWAKILI WA MAADILI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAJUKUMU YA FAMILIA ZAO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here