Home LOCAL WANAWAKE WATAKIWA KUWA MAWAKILI WA MAADILI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAJUKUMU YA FAMILIA ZAO.

WANAWAKE WATAKIWA KUWA MAWAKILI WA MAADILI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAJUKUMU YA FAMILIA ZAO.

Na: Maiko Luoga, TANGA. 

Wanawake Mkoani Tanga wametakiwa kuwa mawakili wema wa kuelimisha jamii hasa Vijana wa kike na wakiume ambao maranyingi wanaishi na kufuata maadili mabovu na kuacha misingi na tamaduni bora zilizo asisiwa na wazee nchini ikiwemo wazazi wao.

Wito huo umetolewa Juni 24, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Mhe, Sirieli Mchembe wakati akizungumza na Wanawake wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Tanga kwenye Mkutano Mkuu wa Ushirika wa Mama wa Kikristo UMAKI uliofanyika Wilayani Handeni na kuwakutanisha mamia ya Wanawake.

“Mwanamke usifurahi kuona Mtoto wa mwenzako akiharibikiwa tumia nafasi hiyo kupiga magoti na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili abadilike, kwakuwa sisi ni ndugu” Mhe, Sirieli Mchembe DC Handeni Mkoani Tanga akizungumza na Wanawake wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha Wanawake kuheshimu familia zao ikiwemo waume wa watoto ili kuimarisha umoja na upendo kwenye ndoa zao, kulitumia Kanisa kufanya maombi ya kuliombea Taifa na Viongozi wake sambamba na kujiimarisha kiuchumi ili kuondokana na kuwa tegemezi kwa waume zao.

“Mwanamke wa kikristo unatakiwa kuwa mfano katika jamii Ili wengine waishi kupitia wewe, unakuta Kanisani unaonekana mwema lakini kwenye familia yako unatia aibu hii si sawa tubadilike Wanawake wenzangu” Mhe, Sirieli Mchembe DC Handeni Mkoani Tanga.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu tangu niteuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya hii hili ni tukio langu la kwanza la kazi ambalo nafanya nikiwa nanyi Wanawake wenzangu tena tukio la kumtukuza Mwenyezi Mungu nimefarijika Sana ndio maana nilisema lazima nifike” Mhe, Sirieli Mchembe DC Handeni Mkoani Tanga.

Bw, Mashaka Mgeta Katibu Tawala Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga amewataka Wanawake hao pamoja na kushiriki matukio ya ibada kuhakikisha wanatumia muda wao kufanya kazi pamoja na kutumia muda mwingi kujenga misingi ya maadili katika familia.

Bi, Magreth Ndonde Massawa Katibu wa UMAKI Kanisa Anglikana Tanzania na Bi, Joyce Mhando Katibu wa UMAKI Dayosisi ya Tanga licha ya kushukuru ushiriki wa Mkuu wa Wilaya wamesema, Mkutano huo mkuu utafanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa UMAKI Dayosisi ya Tanga na baadhi ya viongozi wengine wa Dayosisi hiyo.
Previous articleRC SENDIGA KUZINDUA USAFI MANISPAA YA IRINGA
Next articleBRELA YAWAPIGA MSASA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here