Home LOCAL RC MAKALLA AWAOMBA MADIWANI KUMUUNGA MKONO KWENYE AJENDA YA USAFI DAR ES...

RC MAKALLA AWAOMBA MADIWANI KUMUUNGA MKONO KWENYE AJENDA YA USAFI DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaomba madiwani na Wenyeviti wa mtaa kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii katika Suala la usafi.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo katika kikao Cha madiwani na watendaji kata manispaa ya Temeke katika ziara yake ya kujitambulisha na kueleza vipaumbele kwa mkoa wa dar es salaam ambapo amewaeleza madiwani na watendaji nanma ambavyo haridhishwi na Hali ya usafi Dar es salaam na kuwaomba kumuunga mkono kuiliweka jijii Safi.

Aidha RC Makalla ameeleza mpango wake wa kupendezesha mandhari ya mkoa, kuwapanga vizuri wamachinga na  kuondosha magari mabovu yanayoharibu mandhari ya jiji hilo.

Katika kikao hicho RC Makalla pia amewapa vipaombele vya kushughulikia ikiwemo Ulinzi na Usalama, Usimamizi miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa Mapato, utatuzi wa kero za Wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano.
Previous articleKUTANA NA KAMPUNI YA LAZARO ENERGY GROUP WABUNIFU WA MAJIKO MBADALA KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
Next articleBRELA YAWANOA MAAFISA BIASHARA KUTOKA MIKOA YA IRINGA, RUVUMA NA NJOMBE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here