Home BUSINESS KUTANA NA KAMPUNI YA LAZARO ENERGY GROUP WABUNIFU WA MAJIKO MBADALA KWA...

KUTANA NA KAMPUNI YA LAZARO ENERGY GROUP WABUNIFU WA MAJIKO MBADALA KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Tanzania  ni miongoni mwa nchi  ambazo hivi karibuni zimeadhimisha siku ya mazingira Duniani ambapo kitaifa zilifanyikia katika viwanja vya Mnazi mmoja vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika maadhimisha hayo viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa walipata fursa ya kuhudhuria na kutoa neno kuhusu siku hiyo ya mazingira duninia lakini pia mashirika ,taasisi na wadau wengine na wenyewe hawakubaki nyuma nao washiriki.

Waziri Mwenye dhamana na utunzaji waazingira kutoka katika ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Seleman Jafo ni miongoni mwa watu ambao walitoa neno na maagizo ya  kuhimiza watanzania juu ya  umuhimu wa kutunza mazingira yanayowazunguka lakini ukataji miti  na matumizi ya kuni.

Katika siku hiyo ya mazingira pia Mjasiliamali Lazaro Mathias ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Lazaro Energy Group naye alishiriki huku akiwa na Nishati mbadala ambayo imetokana na malanda ya mbao

Akiwa katika mwaliko wa Serikali alifika katika viwanja vya Mnazi mmoja na kupata wasaa wa kuonyesha majiko ya kupikia ya kisasa ambayo yanatumia nishati mbadala kwa maana ni kuni ambazo zimetengenezwa Kwa utalamu wa hali ya juu kupitia mtambo wa kisasa.

Mathias ambaye pia kupitia Kampuni yake ya Lazaro Energy Group inamiliki kiwanda cha kuchana na kupasua mbao,na malanda yanayotokana na mbao hizo ndio zinatengeneza kuni kwa ajili ya kupikia.

Mathis anasema aliumiza kichwa kwa muda mrefu namna ya kubadilisha malanda na kuwa nishati ya kuni ambayo haiwezi kuwa sehemu ya uhalibifu wa Mazingira.

Kupitia siku ya mazingira.

Mathias ambaye ni mkazi wa Tegeta Wilayani kinondoni anasema kuwa kupitia siku ya Mazingira Duniani Kwa mwaliko aliopewa na mamlaka husika alionyesha  kuni kama  nishati  mbadala na majiko yake ambayo yanatumika Kwa kupitia kuni hizo.

Anasema licha ya majiko hayo kuwa machche lakini wananchi wameonyesha kushawishika nayo nakwamba yanaweza kawa na msaada mkubwa katika Mapambano dhidi ya utunzaji mazingira .

Awali katika mahojiano na Mwandishi wa makala  haya anasema kuwa Kampuni yake mbali na mambo mengine lakini ina jihusisha na kutengeneza thaman mbalimbali na biashara hiyo ndio aliaza Kwa miaka iliyopita na Siku za hivi karibuni ameleta mtambo Kwaajili ya kutengeneza kuni ambazo ni nishati mbadala kwa matumizi ya jikoni.

Anasema kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni njia moja wapo ya kulinda mazingira ambapo malanda ya mbao yanayotoka katika kiwanda ndio  yanatumika kutengenezea kuni mbadala ambazo pia zinatumika kupikia majiko ya kisasa wanayoyatengeneza.


Kuhusu maono.

Mathias ambaye pia ndio Mkurugenzi wa Lazaro Energy Group anasema msukumo wa kuleta mtambo wa kisasa Kwa ajili ya kutengenezea nishati hiyo mbadala ilitokana na uwepo wa malanda hayo  ambayo alikuwa anaumiza kichwa namna ya kuyatumia.

Anasema baada ya kupatikana Kwa  mashine  (mtambo ) ndio wakaaza kutengeneza kuni ambazo pia zinakwenda kutumika katika majiko wanayotengeneza tena Kwa utalaamu wa hali ya juu. huku akiwaalika Mawaziri wa wizara mbili hadi tatu kwenda kuona ili kutoa fursa kwake ya kutengeneza zaidi Kwa ajili ya matumizi ya Taasisi husika wanazozisimamia.

Ametoa mfano wizara ya elimu Kwa Shule za Boding wanaweza kununua majiko hayo ya kuni mbadala na kutumia kuivisha chakula lakini wizara ya uwekezaji Kwa ajili ya kumtafutia masoko zaidi na wizara ya Viwanda Kwaajili ya kumuongezea utaalamu au ujuzi.

 Akizungumzia ushirikiano anaopata .

Mkurugenzi huyu anasema ushirikiano kutoka kwenye mamlaka  bado si mkubwa japo jitihada zinafanyika hasa Serikali ya mtaa wa Tegeta kuzitaka wizara husika kusaidia ubunifu mkubwa ambao umefanyika juu ya kupambana na uhalibifu wa mazingira.

Kuhusu uzalishaji na utengenezaji wa  majiko.

Mathias anasema uzalishaji bado ni mdogo lakini huko mbeleni  wanakoelekea  anaamini utaongezeka na kudai  hata hivyo  utafiti wa kibiashara bado hawajafanya wa kutosha ambao unawapelekea  wao  kuongeza uzalishaji wa kutosha  utakaoleta faida .

Kuhusu walengwa wa majiko hayo.

Anasema kimsingi wao kama Lazaro Energy Group wamezilenga zaidi taasisi za Serikali kama vile taasisi za shule ,vyuo pamoja na watu binafsi  kuweza kununua majiko hayo yenye ubora huku akiwataka kujitokeza Kwa kuweka oda ya kutengenezewa Kwa ajili ya matumizi.

Anashauri Serikali   kutokana na jitihada ambazo wao wanazifanya za kupambana na uhalibifu wa Mazingira na kufikia hatua ya kutengeneza majiko yanayotumia Nishati mbadala nivema ikaunga mkono kwa kuwafikia nakuona hali halisi .

“Tunahitaji mtambo mwingine wa kisasa  Kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi kwani Kwa sasa uwezo wao wakifedha ni mdogo mno.nakutoa wito Kwa taasisi za fedha kupunguza gharama za liba ili kutoa nafasi ya kuweza kukopa.

Anasema gharama za riba zinakuwa juu hivyo nivema wakaliona hilo, kwani wakipunguza na kuwa rafiki Kwa wahitaji mikopo basi wanaweza kukopa ili kuongeza vifaa vya kisasa Kwa ajili ya shughuli zao.

Mathias anatumia Makala haya kuwaomba wadau na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi katika kukabiliana  na uhalibifu wa Mazingira nivema Jamii sasa ikapokea ushauri wa kutumia nishati  mbadala na hata gharama zake ziko chini sana ukizingatia majiko yanauwezo wa kutumika Kwa miaka zaidi ya 50.

Kuhusu changamoto.

Kwaupande wake Mhandisi David Lazaro  ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi, anasema changamoto kubwa kwao ni  kwenye kuunda kwasababu gharama za uendeshaji ni kubwa  mno ambapo inahitajika nguvu kazi  ya kutosha  Kwa maana ya wafanyakazi.

Pia changamoto nyingine wanayokutana nayo ni matumizi ya umeme hayaendani na pato wanalopata kwani Kwa mwezi wanatumia sh. 800,000 nakwamba licha ya uendeshaji kuwa na gharama lakini ndoto yao au malengo yao ni kusaidia jitihaza za Serikali katika kulinda mazingira .

Anasema nivema Serikali ikawaongeza nguvu japo kidogo ili wao kama Lazaro Energy Group waendelee kutengeneza nishati mbadala  Kwa manufaa ya Taifa Kwa ujumla na Duniani.

Kuhusu vijana wanaotoka vyuoni.

David anasema kuwa vijana nivema wakajitambua tu kwani hata yeye ni kijana lakini amepima Maji hivyo ameamua kuondoa fikra za ajira na badala yake ameamua  kujiajiri nakwamba kujiajiri kunahitaji uthubutu ,uvumilivu.

“Hapa natoa wito Kwa vijana wasibweteke tu na kusubiri ajira badala yake  wajiajiri na wala hakuna kuleta kisingio cha kukosa mtaji lakini kitu cha muhimu kichwani ni kuwa na wazo kabla ya kupata hela ” anasema

Anasema licha ya kutengeneza nishati mbadala pamoja na mbao lakini pia kupitia kampuni hiyo wanajishughulisha na kilimo cha zao la chikichi ambalo linatoa mafuta ya mawese.

Kuhusu majiko anasema yana uwezo wa  kudumu Kwa zaidi ya miaka 50 lakini pia nivipande sita tu vya kuni nishati mbadala vinaivisha mchele kilo 50 hivyo Kwa sababu Shule ni taasisi za umma ambazo zipo chini ya Serikali anawaomba wachangamkie fursa ya bidhaa hiyo.

“Kwakweli tunandoto ya kufanya Jambo kubwa sana na hasa Vita dhidi ya uhalibifu wa mazingira hakuna ubishi kwamba changamoto ya mazingira imekuwa ni  kubwa na inakwenda Kwa kasi  hata huko  duniani hivyo elimu juu ya mazingira lazima tuendelee kutoa hususani kubuni njia Mbagala za kukabiliana nazo.


Anamaliza Kwa kuziomba Taasisi za umma na binafsi kama vile mashuleni .hosipatli na vyuo kufika katika ofisi yake iliyopo Tegeta kituo cha Azania nyumba plot no 5 na block Namba HL utakuwa umefika  Lazaro energy group ili kujipatia thaman ,majiko na Mafuta ya mawese.

Au unaweza kuwasiliana nao kwa namba za simu zifuatazo.

+255 782 011844

+255 767 618333

+255 714 250307

Barua pepe: mathiasdavid70@gmail.com

                      mathiasdavid70@yahoo.com

Mwisho.

  

Previous articleBALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI
Next articleRC MAKALLA AWAOMBA MADIWANI KUMUUNGA MKONO KWENYE AJENDA YA USAFI DAR ES SALAAM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here