Home BUSINESS BRELA YAWANOA MAAFISA BIASHARA KUTOKA MIKOA YA IRINGA, RUVUMA NA NJOMBE.

BRELA YAWANOA MAAFISA BIASHARA KUTOKA MIKOA YA IRINGA, RUVUMA NA NJOMBE.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia mafunzo ya BRELA.

NJOMBE
.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),  inatoa mafunzo kwa maafisa biashara kuhusu Sheria ya Leseni za Biashara pamoja na taratibu za utoaji wa leseni hizo. Mafunzo  hayo yaliyoanza rasmi Juni 14, 2021 katika ukumbi wa Milimani Motel mkoani Njombe, yameshirikisha Maafisa Biashara kutoka mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma

Afisa Leseni Mwandamizi  kutoka BRELA Bw. Abas Cothema amesema lengo kuu la kuandaa mafunzo  hayo ni kutoa elimu na hamasa kwa Maafisa Biashara ambao wamekuwa ni wadau wakubwa wa BRELA. 

Amesema BRELA  imejipanga kuwafikia Maafisa Biashara kote nchini na kuwapa elimu juu sheria za utoaji wa Leseni  za Biashara, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za sheria hiyo ili   kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufasaha zaidi.

Bw.Cothema amesema mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa BRELA  wa kupunguza na hatimaye kuondoa  tatizo la vishoka wanaokwamisha taratibu za upatikanaji wa Leseni kwa wafanyabishara.

Naye Afisa Biashara kutoka Mkoa wa Njombe Bw. Lusungu Essau Mbede licha ya kupongeza juhudi zinazofanywa  na BRELA alieleza kuwa kumekuwa na changamoto kwa upande wa wafanyabiashara kwani baadhi yao hawana uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu leseni na  kushindwa kufuatilia kwa  wakati leseni hizo. 

Nimefurahi kuwaona BRELA kwa kutukutanisha Maafisa Biashara wa Mikoa mitatu (Njombe, Iringa na Ruvuma) na kutupatia mafunzo haya muhimu”, alisema Bw. Lusungu Essau Mbede.

Mafunzo haya ya siku tano yanatarajia kuhitimishwa Juni 18, 2021.
Previous articleRC MAKALLA AWAOMBA MADIWANI KUMUUNGA MKONO KWENYE AJENDA YA USAFI DAR ES SALAAM
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TANO JUNI 16-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here