Home INTERNATIONAL MWILI WA MZEE KAUNDA KUAGWA KATIKA MIKOA KUMI YA NCHI HIYO.

MWILI WA MZEE KAUNDA KUAGWA KATIKA MIKOA KUMI YA NCHI HIYO.

LUSAKA, Zambia

SERIKALI ya Zambia imetangaza ratiba ya mazishi ya mwili wa mwasisi wa taifa hilo, Dk. Kenneth Kaunda, aliyefariki dunia Juni 17, mwaka huu.

Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Inonge Wina,  amesema ratiba hiyo imeanza Juni 23, 2021 kwa mwili wake kuzungushwa katika mikoa 10 ya nchi hiyo ili kuwapa fursa wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Amesema wakati mwili huo ukiagwa, taifa litaendelea kuwa katika maombolezo ya  siku 21 na kituo cha taifa cha televisheni kitarusha moja kwa moja matukio yote.

Makamu huyo wa Rais wa Zambia, amesema msafara wa mwili wa Kaunda utapita katika makao makuu ya mikoa pekee.

Previous articleWAZIRI SIMBACHAWENE AINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI JESHI LA MAGEREZA, WANANCHI CHIHIKWI, MSALATO JIJINI DODOMA
Next articleCLOCK TOWER MARATHON YAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA SASA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 8 MWAKA HUU, MEYA ASEMA YATAFUFUA UTALII.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here