Home SPORTS SIMBA SC YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA ROBO FAINALI, YAFUNGWA 4-0 NA...

SIMBA SC YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA ROBO FAINALI, YAFUNGWA 4-0 NA KAIZER CHIEFS.

JOHANNESBURG

TIMU ya wekundu wa msimbazi Simba SC imepoteza mchezo wake wa ugenini wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kupokea kipigo cha mabao 4-0 na timu ya Kaizer Chiefs ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali katika Dimba la FNB Jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Mlinzi wa kati wa Kaizer Chiefs Eric Mathoho aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 6 ya mchezo huo, huku Samir Nurkovic akipachika mabao mawili katika dakika ya 34 na 57 ya mchezo huo ambapo David Leonardo Castro Cortés akipigikia msumari wa mwisho na kuongeza goli la nne Katika dakika ya 63 ya mchezo huo.

Mchezo wa marudiano utafanyika Jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi ijayo tarehe 22 ambapo Simba SC watahitajika kushinda mabao 5-0 ili kuweza kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ALIVYOHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUHIGWE
Next articleLEICESTER CITY YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA FA ENGLAND YAICHAPA 1-0 CHELSEA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here