Diwani wa Viti Maalum Wanawake halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Batuli Mziya akichangia hoja katika baraza la Madiwani halmashauri ya jiji la Dar es salaam (Picha na Heri Shaaban) |
Diwani wa Kata ya Mzinga JOB ISACK akielezea kero za kata yake kuhusiana na eneo la shule lililovamiwa na WANANCHI kugeuza makazi yao (Picha na Heri Shaaban) |
(PICHA NA HERI SHAABAN).
Na: Heri Shaaban, DAR ES SALAAM.
MADIWANI wa halmashauri ya Jiji la Dar es salaam waitolea kilio chao Wakala wa Barabara Mijini na Vijini TARURA kutokana na ubovu wa barabara za jiji hilo.
Madiwani hao walitoa kilio chao katika kikao cha Baraza madiwani leo ukumbi wa Arnatogluo wilayani Ilala.
Akizungumza katika baraza hilo Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangomo , aliwataka TARURA watoe maelezo kutokana na kukitekeleza kipande cha Barabara ya Balakuda Vingunguti na kusababisha kero ya kukata mawasiliano.
“Tunapata shida kwa kushindwa kuwapa majibu wapiga kura wetu kutokana na kero ya Barabara WANANCHI wangu zaidi ya 20,000 wanashindwa kutumia barabara hiii kutokana na maandaki “alisema Alice
Alice aliwataka TARURA kutengeza barabara zilizo chini yao zote ili kuondoa changamoto wanazokumbana nazo wananchi.
Kwa upande wake Diwani wa Kinyelezi Leah Mgitu alishauri halmashauri Jiji la Dar es salaam waunge mkono juhudi za Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwamba halmashauri zenye uwezo washirikiane na TARURA kujenga Barabara ili kutatua kero za wananchi.
Aidha Diwani Leah alimuomba Mkurugenzi wa Jiji aeleze katika baraza hilo kuhusu eneo la Kifuru ambalo mwananchi amelipwa fidia lakini ujenzi wa shule bado kuanza mpaka sasa.
Naye Diwani wa Mzinga JOB ISACK alisema eneo la kata ya Mzinga wananchi 82 wamevamia eneo la huduma za Jamii ambalo limetengwa kwa ajili ya Shule ya kata ambapo wamejenga nyumba mpaka sasa ajajua ufumbuzi wake kutokana na kuwepo kwa wanafunzi wengi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali mpango wa elimu bure.
Mhandisi wa Barabara wa TARURA Wilaya Ilala Road Muniko alisema kipande cha Barabara Barakuda Vingunguti taratibu zimeshaanza kwa ajili ya kujenga kipande hicho.
Mhandisi Muniko alisema changamoto kubwa ni bajeti ndogo wanashindwa kufikia barabara zote kwa wakati na bajeti iliyopita kwa sasa ndio imepitishwa na madiwani waliopo.
Baraza la Madiwani wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam liliongozwa na Mwenyekiti wake Meya wa Halmashauri hiyo Omary Kumbilamoto na Kaimu Mkurugenzi Tabu Shaibu.
Mwisho.