Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari. |
Evans Rubara kutoka FADev akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari |
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo. |
Waandishi wahabari katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama pamoja na watoa Mafunzo kutoka FADev
Na,Saimon Mghendi, Kahama. |
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha, ameipongeza taasisi ya FADev kwa kuwapa mafunzo waandishi wahabari yanayohusiana na sekta ya wachimbaji wadogo wa madini, Jambo ambalo litawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi wakati watakaapokua wanandika habari zinazohusiana na wachimbaji wadogo nchini.
Macha ameyasema hayo leo wakati alipokua akifungua semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari ya siku nne yalioandaliwa na taasisi ya kuendeleza wachimbaji wadogo nchini ya FADev, Katika ukumbi wa Hoteli ya Submarine katika Manispaa ya Kahama.
Mafunzo hayo ya siku nne yanayotolewa na taasisi ya FADev kwa waandishi wa habari, yanajumuisha waandishi wa habari wa kutoka mikoa mitatu, ambayo ni Shinyanga,Geita pamoja na Mwanza.