Home LOCAL MAKAMBA AANZA KAZI RASMI WIZARA YA NISHATI

MAKAMBA AANZA KAZI RASMI WIZARA YA NISHATI


Waziri wa Nishati, January Makamba (aliyeshika Ua) baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mji wa Magufuli Mtumba tayari kuanza majukumu yake mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo, Septemba 13, 2021, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.

Waziri wa Nishati, January Makamba akisalimiana na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara hiyo mara baada ya Waziri huyo kuapishwa kushika wadhifa huo na kuwasili wizarani hapo, Septemba 13,2021.

Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato( Pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja (wa Pili kulia), na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ( kulia), wakibadilishana Mawazo mara baada ya Waziri huyo kuapishwa kushika wadhifa huo na kuwasili wizarani hapo, Septemba 13,2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja (aliyesimama )kumkaribisha Waziri wa Nishati, January Makamba katika kikao cha Waziri huyo na Uongozi wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara mara baada ya Waziri huyo kuapishwa kushika wadhifa huo na kuwasili wizarani hapo, Septemba 13,2021.



Waziri wa Nishati, January Makamba (katikati mstari wa mbele),akiwa katika picha ya pamoja viongozi waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo baada ya kumaliza kikao chake na uongozi huo baada ya kuapishwa kushika wdhifa huo, Septemba 13,2021.

Na: Zuena Msuya na Hafsa Omari, DODOMA.

Waziri wa Nishati, January Makamba, ameanza kazi rasmi katika wizara hiyo kwa kuwataka watendaji wa wizara hiyo pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa weledi wa uaminifu na uadilifu kwa maslahi mapana ya Taifa.

Amesema hayo wakati akizungumza na Uongozi wa Wizara hiyo pamoja Taasisi zilizo chini yake, mara baada ya  kushika wadhifa huo na kuwasili katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Magufuli Mtumba, Septemba 13, 2021.

Aliwaeleza watumishi hao kuwa anahitaji kuona matokeo chanja katika utendaji kazi pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Leonard Masanja, Naibu Katibu Mkuu, Kheri Mahimbali, Viongozi Waandamizi wa wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo.

Aidha, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kusukuma mbele Sekta ya Nishati kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi na kukuza uchumi wa Taifa kwakuwa sekta hiyo ni muhimili muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Sambamba na hilo amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo,ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini( REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji( Ewura), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja( PBPA) Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Mafuta( PURA),kuhakikisha zinafanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya nchi na watanzania kwa jumla.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato alitoa pongezi kwa Waziri Nishati kwa kuaminiwa na kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Mhe. Samia Suluhu Hasani na kwamba watumishi wa Wizara wamempokea kwa moyo mkunjufu.

Vilevile alimuhakikishia Waziri Makamba, kuwa watumishi wa Wizara pamoja na Tasisi zilizo chini ya wizara hiyo zitatoa ushirikiano mkubwa wa kiutendaji katika kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele na kunufaisha Taifa na watanzania kwa jumla.

Previous articleSIMBA KUENELEA KUWAWEKA FITI WACHEZAJI WAKE KWA MECHI ZA KIRAFIKI
Next articleHABARI KUU MAGAZETI YA LEO J.NNE SEPTEMBA 14-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here