Home LOCAL SERIKALI YATOA MSIMAMO WA CHANJO NCHINI

SERIKALI YATOA MSIMAMO WA CHANJO NCHINI

Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Melezo Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo June 5,2021 jijini Dodoma kuhusiana na masuala mbalimbali ya Nchi.  

DODOM.

SERIKALI  inaendelea kuwahimiza Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali kwa juhudi na maarifa huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona, zikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka.

Hayo yamesemwa jana jijini hapa Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Melezo Gerson Msigwa wakati akiongea na vyombo vya habari ambapo amesema Serikali imeamua kuimarisha juhudi za kupambana na janga hilo kwa kutoa nafasi kwanza kwa Wataalamu wakiongozwa na Prof. Said Aboud kufanya tathmini ya kitaalamu na kuishauri Serikali juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Aidha ameeleza kuwa Balozi na Taasisi mbalimbali za Kimataifa zimeruhusiwa kuleta chanjo kwa ajili ya raia wa nchi zao na watumishi wao kwa ajili ya kufanya Balozi na Taasisi hizo kuendelea na kazi zao kama kawaida .

“Tunamshukuru Mungu madhara ya ugonjwa huu kwa nchi yetu hayakuwa makubwa kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani,Tanzania inachukua tahadhari huku ikihakikisha hatua zinazochukuliwa haziathiri uchumi,”alisema.

Msigwaamesema kuwa kwenye eneo hili la ugonjwa wa Corona kumekuwa na maneno mengi na kujazana hofu bila sababu kuutaka Umma kuacha Kamati imefanya kazi yake na imewasilisha mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

“Jana Mhe. Rais amekabidhiwa mapendekezo hayo yenye mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona (Covid-19) na mapendekezo ya mpango kazi wa uratibu wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo yaliyowasilishwa na kamati ya wataalamu aliyoiunda kwa ajili ya kuishauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo,”amefafanua.

Hata hivyo Msemaji huyo wa Serikali amesisitiza kuwa Mhe. Rais ameelekeza mapendekezo hayo sasa yaandikiwe andiko na yawasilishwe katika Baraza la Mawaziri ili kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi na baada ya hapo Serikali itakuja na tamko juu mapendekezo hayo.

Akizungumzia hali ya Uchumi amesema kuwa ni nzuri japo kwa upande wa Tanzania tumepatwa na madhara ya Corona kama ilivyo kwa nchi zingine Duniani ambapo kwa Tanzania  ulikuwa unakua kwa wastani wa asilimia 6.9 na  umeshuka hadi wastani wa asilimia 4.7, na matarajio ni kuwa uchumi  utaendelea kukua vizuri kutokana na hatua madhubuti ambazo zimechukuliwa.

Licha ya hayo ameeleza kuwa Mfumuko wa bei kwa sasa ni wastani wa asilimia 3.3% ambayo ni kiasi kizuri huku Akiba ya fedha za kigeni ni nzuri ambazo zinatosha kununua bidhaa na huduma kwa muda wa zaidi ya miezi 4.7.

Kuhusu Maendeleo ya Miradi ya kimkakati Msigwa amesema Reli ya kisasa/Standard Gauge Railway (Dar es Salaam – Morogoro (km 300) 91%, Morogoro – Makutupora (km 422) 61% na ujenzi wa reli Mwanza – Isaka umeanza ambapo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 372.34 za ujenzi wa kilometa 341 za reli hiyo.

Msigwa amesema kuwa kwa upande wa  huduma za afya nchini ,Serikali imetoa shilingi Bilioni 121.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa zinazokwenda katika mikoa mbalimbali na kwamba  hii ni sehemu ya ile bajeti kubwa ya shilingi Bilioni 270 za dawa na vifaa tiba.

Amesema Magari ya wagonjwa (Ambulace) 20 yamenunuliwa na kugawiwa kwa mikoa 16 huku Huduma za matibabu ya kibingwa zikiwa zinaendeleaKuhusu ukusanyaji kodi Serikali imekusanya kodi vizuri,  na zipo hatua madhubuti zilizochukuliwa kurekebisha dosari zilizokuwepo katika jukumu zima la ukusanyaji wa kodi baada ya maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Rais.

“Wote mlimsikia Mhe. Rais akiagiza ukusanyaji wa kodi ufanyika kitaaluma badala ya kutumia mabavu. Mnafahamu kumekuwa na vikosi kazi (task force) ambavyo vilitumika kukusanya kodi katika baadhi ya maeneo. Vikosi kazi hivi vimeondolewa na Watanzania wanalipa kwa utaratibu wa kawaida wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)”amesema na kuongeza,.

Credit – Fulshangwe Blog.

Previous articleUN KUSAIDIA UTEKELEZAJI MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA NCHINI
Next articleKUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA MHE, EDWIN SWALLE ASIMAMA NA WANANCHI WA LUPEMBE, ASHAURI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI,

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here