MZEE DAVID CLEOPA MSUYA AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya kilichotokea leo tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo. kufuatia kifo hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu...
SERIKALI KUENDELEA KUKARABATI VITUO VYOTE KONGWE, VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
http://SERIKALI KUENDELEA KUKARABATI VITUO VYOTE KONGWE, VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYAOR - TAMISEMI Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesema itaendelea kukarabati hospitali zote Kongwe kupitia mpango mkakati wa ukarabati, na upanuzi wa hospitali kongwe za halmashauri ,vituo vya afya Pamoja na zahanati ili kuboresha miundombinu ya huduma za afya kote nchini. Hayo yamesemwa leo Mei 07, 2025 bungeni Jijini...
HOSPITALI ZA BENJAMIN MKAPA, MLOGANZILA KUENDELEA KUTUMIKA KAMA VITUO VYA MAFUNZO UDOM NA MUHAS
Na, WAF-Dodoma Serikali imesema Hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Mloganzila zitaendelea kuwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya kwa madhumuni ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kuboresha ubora wa huduma sambamba na kutumika kama vituo vya mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya Vikuu vya Dodoma na Muhimbili. Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,...
KERO YA MAJI KIJIJI CHA MLOKA, MBUNJU MVULENI NA NDUNDUTAWA YAPATIWA UFUMBUZI
Na. Mwandishi Wetu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya Maji itakayojengwa katika Vijiji vitatu vya Mloka, Mbunju Mvuleni pamoja na Ndundutawa ambayo itahudumia Wananchi 16, 593 hali itakayosaidia kupunguza kero ya Maji katika maeneo hayo. Meneja wa Wakala wa Maji na...
MHE- ZAINABU ATEMBELEA BANDA LA TAMISEMI KONGAMANO LA KIMATAIFA NA MAONESHO YA ELIMU MTANDAO- DAR ES SALAAM.
Naibu Waziri anayeshughuhulikia Elimu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Zainab Katimba atembelea banda la TAMISEMI kwenye Kongamano la Kimataifa na Maonesho ya Elimu Mtandao Jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Zainab Katimba ametembelea banda la maonesho la Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwenye Kongamano la 18 la kimataifa na Maonesho ya Elimu Mtandao, Mafunzo na Maendeleo ya Kukuza Ujuzi yanayoendelea katika Ukumbi...
NHIF SASA KUGHARAMIA MATIBABU YA AFYA YA AKILI, KUFUATA MWONGOZO
Na WAF, DODOMA Serikali imesema huduma za afya ya akili zimeshajumuishwa kwenye vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na hivyo wananchi wanaonufaika na bima wanaweza kupata matibabu hayo kwa mujibu wa mwongozo wa matibabu uliopo. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, huduma za afya...