Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo akizungumza katika hafra ya kuhitimisha mashindano ya michezo ya vijana chini ya Miaka 15 yaliyoandaliwa na Mgodi wa GGML.
Mkurugenzi wa Mgodi wa GGML Terry Strong
Na. Costantine James, Geita
Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amewataka wazazi wilayani humo kuwasimamia vyema watoto wadogo katika maeneo yanayozungukwa na migodo kwa lengo la kuwaepusha na shughuli za migodini wakiwa bado na umri mdogo.
Shimo amesema hayo katika hafla ya kuhitimisha mashindano vijana chini ya miaka 15 yaliyoandaliwa na mgodi wa GGML yaliyolenga kuhamasisha kuwaweka watoto mahala salama ili kuwaepusha na shughuli mbalimbali za migodini.
Amesema watoto bado wanaonekana katika maeneo ya migodini wakifanya shughuli mbalimbali hali inasababisha watoto hao kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu huku wakifanya kazi hizo kinyume na sheria.
Amewataka wazazi na walezi wilayani humo kuhakikisha wanawalinda na kuwatunza watoto ili wasijihusishe na shuguli za migodini na badala yake wajikite katika masomo kwani kufanya shughuli za mogodini ni kosa kisheria.
Mkurugenzi wa mgodi wa GGML Terry Strong amesema wameamdaa mashindano hayo kwa lengo la kuhamasisha watoto ili wasijikite katika shughuli za migodini na badala ake wajikite katika masomo.
Amesema wameandaa michezo hiyo kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kiasi gani maeneo ya uchimbaji sio salama kwa watoto pamoja na kuendeleza kuhamasisha watoto wapende shule na kuboresha michezo mashuleni.