Home BUSINESS DC SHIMO AWATAKA WAZAZI KUWACHUNGA WATOTO SHUGHULI ZA MIGODINI

DC SHIMO AWATAKA WAZAZI KUWACHUNGA WATOTO SHUGHULI ZA MIGODINI

Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo akizungumza katika hafra ya kuhitimisha mashindano ya michezo ya vijana chini ya Miaka 15 yaliyoandaliwa na Mgodi wa GGML.

Mkurugenzi wa Mgodi wa GGML Terry Strong

Na. Costantine James, Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amewataka wazazi wilayani humo kuwasimamia vyema watoto wadogo katika maeneo yanayozungukwa na migodo kwa lengo la kuwaepusha na shughuli za migodini wakiwa bado na umri mdogo.

Shimo amesema hayo katika hafla ya kuhitimisha mashindano vijana chini ya miaka 15 yaliyoandaliwa na mgodi wa GGML yaliyolenga kuhamasisha kuwaweka watoto mahala salama ili kuwaepusha na shughuli mbalimbali za migodini.

Amesema watoto bado wanaonekana katika maeneo ya migodini wakifanya shughuli mbalimbali hali inasababisha watoto hao kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu huku wakifanya kazi hizo kinyume na sheria.

Amewataka wazazi na walezi wilayani humo kuhakikisha wanawalinda na kuwatunza watoto ili wasijihusishe na shuguli za migodini na badala yake wajikite katika masomo kwani kufanya shughuli za mogodini ni kosa kisheria.

Mkurugenzi wa mgodi wa GGML Terry Strong amesema wameamdaa mashindano hayo kwa lengo la kuhamasisha watoto ili wasijikite katika shughuli za migodini na badala ake wajikite katika masomo.

Amesema wameandaa michezo hiyo kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kiasi gani maeneo ya uchimbaji sio salama kwa watoto pamoja na kuendeleza kuhamasisha watoto wapende shule na kuboresha michezo mashuleni.

Previous articleBRELA, FCC, TIC, WAKUTANA NA WADAU
Next articleWATUMISHI MADINI WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA UWEKEZAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here