Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa mabdiliko ya sheria za habari iliyofanyika Oktoba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim akifuatilia jambo alipokuwa kwenye Warsha hiyo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Katika kuhakikisha kunakuwepo na ushawishi mkubwa kwa watunga sheria kufanya marekebisho ya sheria ya habari, waandishi wa habari nchini wametakiwa kujua sheria zinazoongoza tasnia ya habari ili kupata wigo mpana wa kufahamu upungufu uliopo kwenye sheria hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wahariri juu ya mipango ya uchechemuzi wa mabdiliko ya sheria za habari iliyofanyika Oktoba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.
Salim amesema kuwa bado waandishi hawajapata uelewa mpana juu ya sheria ya habari hususan vifungu vyenye ukakasi vinavyopaswa kubadilishwa na kwamba jutihada za makusudi zinahitajika kuhakikisha waandishi wanaifahamu sherianhiyo.
Ameongeza kwamba, ikiwa waandishi wakiijua vizuri sheria hizo na upungufu wake, ataweza kuandika habari kwa upana zaidi bila wasiwasi wowote na kuizungumzia mahali popote anapokutana na makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo Wabunge.
“Bado waandishi hatujawa na uelewa mpana wa sheria zinazotuhusu, tufanye jitihada kuzijua. Tuwashawishi wenzetu juu ya sheria zinazokwaza ukuaji wa tasnia ya habari na maendeleo ya Taifa,” amesema.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeandaa Warsha ya siku mbili kwa waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwezo juu ya uandishi wa utetezi wa mabadilko ya Sheria ya Vyombo vya Habari.