Home LOCAL WAKUFUNZI WA MIKOA WAPATIWA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA EBOLA

WAKUFUNZI WA MIKOA WAPATIWA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA EBOLA

Na. WAF – Morogoro

Wakufunzi wa mikoa nchini ambao ni wataalamu wa Afya kutoka katika hospitali ya Taifa, hospitali za kanda, hospitali maalumu na hospitali za Rufaa za Mikoa wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na Ebola.

Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Erick Richard amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwatayarisha wakufunzi hao kukabiliana na Ebola na wanaporudi kwenye Mikoa yao kwenda kutoa elimu hiyo kwa watoa huduma ya Afya.

“Wakufunzi hawa tumewafundisha jinsi ya kutambua na kutibu pamoja na kuweza kutumia afua mbalimbali za kujikinga ili waweze kumhudumia mgonjwa wa Ebola pindi anapogundulika bila ya wao kupata maambukizi.” Amesema Dkt. Richard

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) wameleta wataalamu wa magonjwa ya Milipuko kutoka nchi ambazo zilishawahi kutokea kwa mlipuko wa Ebola ikiwemo nchi ya Congo DRC, Zambia, Bukinafaso, Cameron, Sierra-Leone kuja kutoa mafunzo hayo nchini.

“Ugonjwa huu hadi sasa haujaingia nchini lakini tumejiandaa na mafunzo haya kuwa ni sehemu ya utayari katika kujijengea uelewa kwa kuujua ugonjwa wa Ebola na kuutibu, kujikinga na maambukizi na kuzuia maambukizi hayo yasisambae.”Amesema Dkt. Richard

Miongoni mwa mambo waliyofundishwa ni pamoja na kuvaa na kuvua vifaa kinga vya kujikinga na Ebola kwa wahudumu, kupata uelewa wa ugonjwa wa Ebola, Jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi, mafunzo kwa vitendo namna ya kumpokea mgonjwa wa Ebola na kumhudumia.

Mafunzo hayo yamemalizika kutolewa kwa Mikoa yote 28 Tanzania Bara.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

Previous articleMZEE SALIM: WAANDISHI SOMENI SHERIA ZINAZOWAONGOZA
Next articleRAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWAAPISHA WAKILI MKUU WA SERIKALI PAMOJA NA NAIBU WAKILI MKUU WA SERIKALI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here