Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amewahakikishia watanzania kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kufufua viwanda vyote vilivyokufa na kutelekezwa ili viweze kuongeza thamani kwa mazao yanayozalishwa nchini, kutoa ajira
na kuchangia katika ukuaji uchumi kwa ujumla
Waziri Kijaji ameyasema hayo, Oktoba 17, 2022 alipotembelea Kiwanda cha Tumbaku cha Mkwawa kilichopo Mkoani Morogoro kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi baada ya kusimama uzalishajikwa takribani miaka mitatu
Aidha, Dkt. Kijaji amewashauri wakulima wa Tumbaku mkoani humo na Tanzania kwa ujumla kulima tumbaku kwa wingi kwa kuwa zao hilo ni la kimkakati na kwa sasa lina soko ambalo ndio kiwanda hicho cha tumbaku kinachochakata zao hilo na kuviuzia viwanda vya kutengeneza sigara
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bw. Ally Machela amesema kiwanda hicho kuanza kufanya kazi ni neema kwa mkoa huo kwa kuongeza ajira, pato kwa wakulima wa tumbaku na pato kwa taifa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi katika kiwanda hicho Mhandisi Nicholas Kanyamala amesema kiwanda hicho kilichoanza kazi Septemba 2022, kina Uwezo uliosimikwa wa kuchakata tumbaku tani million 65 kwa mwaka ambapo kwa sasa kinachakata tani mil 8 mpaka 10 kwa mwezi na kimeajili wafanyakazi 800 na mwakani kitaajiri zaidi ya 1,000 na kununua tumbaku ghafi tani million 40.