Home BUSINESS SERIKALI IMEJIPANGA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYOKUFA: DKT. KIJAJI

SERIKALI IMEJIPANGA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYOKUFA: DKT. KIJAJI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amewahakikishia watanzania kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kufufua viwanda vyote vilivyokufa na kutelekezwa ili viweze kuongeza thamani kwa mazao yanayozalishwa nchini, kutoa ajira
na kuchangia katika ukuaji uchumi kwa ujumla

Waziri Kijaji ameyasema hayo, Oktoba 17, 2022 alipotembelea Kiwanda cha Tumbaku cha Mkwawa kilichopo Mkoani Morogoro kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi baada ya kusimama uzalishajikwa takribani miaka mitatu 

Aidha, Dkt. Kijaji amewashauri wakulima wa Tumbaku mkoani humo na Tanzania kwa ujumla kulima tumbaku kwa wingi kwa kuwa zao hilo ni la kimkakati na kwa sasa lina soko ambalo ndio kiwanda hicho cha tumbaku kinachochakata zao hilo na kuviuzia viwanda vya kutengeneza sigara

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bw. Ally Machela amesema kiwanda hicho kuanza kufanya kazi ni neema kwa mkoa huo kwa kuongeza ajira, pato kwa wakulima wa tumbaku na pato kwa taifa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi katika kiwanda hicho Mhandisi Nicholas Kanyamala amesema kiwanda hicho kilichoanza kazi Septemba 2022, kina Uwezo uliosimikwa wa kuchakata tumbaku tani million 65 kwa mwaka ambapo kwa sasa kinachakata tani mil 8 mpaka 10 kwa mwezi na kimeajili wafanyakazi 800 na mwakani kitaajiri zaidi ya 1,000 na kununua tumbaku ghafi tani million 40.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 18-2022
Next articleMWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  NDUGU SAMIA SULUHU HASSAN  AFANYA ZIARA FUPI OFISI ZA CCM MKOA WA KIGOMA , LEO OKTOBA 18, 2022.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here