Home LOCAL DKT. BITEKO: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA MWALIMU KATIKA MAENDELEO

DKT. BITEKO: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA MWALIMU KATIKA MAENDELEO

Imeelezwa kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan inautambua mchango wa mwalimu katika kujenga maendeleo ya Taifa.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati wa Sherehe ya Siku ya Mwalimu Duniani iliyoadhimishwa katika wilaya ya Bukombe na kuhudhuriwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Mkoani Geita.

Ameongeza kuwa, mchango wa walimu nchini ni mkubwa katika utoaji wa elimu. Amesema mwalimu ni msingi katika kujenga uchumi.

Naye, Prof. Mkenda amesema katika kusheherekea Siku ya Mwalimu Duniani Serikali itaandaa sherehe hizo ili zifanyike katika wilaya Bukombe Mwaka 2023.

Aidha, ameahidi kujenga Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA katika wilaya ya Bukombe ili kurahisisha kutoa msaada kwa wanachi wa Bukombe na Mkoa wa Geita.

Hafla hiyo imeandaliwa na Chama cha Walimu wilaya ya Bukombe imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ili kusheherekea kwa pamoja siku hiyo muhimu ya mwalimu duniani.

Previous articleRAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI
Next articlePROF. MKENDA SERIKALI KUJA NA MAGEUZI MAKUBWA YA ELIMU NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here