Home LOCAL RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
 
DAR ES SALAAM.
 
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.
 
Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.
 
Tarehe 10 Oktoba 2022 asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili.
 
Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni wake Mhe. Dkt. Ruto.
 
baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Kenya.

 

Previous articleRAIS SAMIA SULUHU AHUTUBIA KATIKA BARAZA LA MAULID KUSHEREHEKEA MAZAZI YA MTUME MUHAMMAD(S.AW)
Next articleDKT. BITEKO: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA MWALIMU KATIKA MAENDELEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here