NA: HERI SHAABAN (ILALA).
BARAZA LA Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamejipanga kwa ajili ya maandalizi ya SENSA ya Watu na Makazi 2022.
Hayo yalisemwa na Kaimu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Saady Khimji Katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji..
“Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tumejipanga vizuri katika maandalizi ya SENSA ya Watu na Makazi 2022 pamoja na Watendaji wa Kata na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wetu”alisema Khimji.
Khimji alisema katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji ajenda kubwa ilikuwa ikijadiliwa suala la SENSA ya Watu Makazi.
Alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika suala la anuani za makazi Wilaya ya Ilala imefanikiwa kufanya vizuri kwa asilimia 100 zoezi la anuani za makazi limekamilika vizuri Kata zote 36.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekuwa akizungumzia umuhimu wa Sensa Watu na Makazi kwa ya Maendeleo ya Taifa na Serikali kwa ujumla .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu alisema maandalizi ya SENSA Wilaya ya Ilala maandalizi yake yamekamilika kuanzia ngazi ya Mtaa Mpaka Kata.
Kaimu Mkurugenzi Tabu Shaibu alisema taratibu zote za SENSA Wilaya ya Ilala zimekamilika na wasimamizi wake Pamoja na Makalani zoezi la uombaji wa AJIRA muda Makalani na Wasaidizi wa sensa limekamilika Mei 19 2022 maombi yaliotumwa Halmashauri 22,561 Kwa nafasi za Makala ni .
Aidha Shaibu alisema wasimamizi wa TEHAMA maombi 19,539 yamekamilika maombi 30,22.hayajakamilika
Mwisho