Home Uncategorized WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI GEITA WATAKIWA KUTUMIA VIFAA VYA USALAMA KAZINI...

WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI GEITA WATAKIWA KUTUMIA VIFAA VYA USALAMA KAZINI ILI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA MAGOJWA.

Na: Costantine James, Geita. 

Wachimbaji  wa Madini Mkoa wa Geita Wameshauriwa kutumia vifaa vya kujikinga katika shughuli za uchimbaji wa madini kwa lengo la kujiepusha na maambukizi ya magojwa mbalimbali yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini.

Akizungumza katika maonesho ya Fahari ya Geita yanayoendelea Mkaoni  Geita Mkurugenzi wa kampuni ya Codeban Company Limited   Baraka Mwakatumba amesema  Uchimbaji wa madini  kwa kutumia vifaa Dhaifu unahatalisha maisha.

Amsema  utumiaji wa vifaa dhaifu katika shughulu za uchimbaji wa Madini unasababisha madhara makubwa ya kiafya hali inayosababisha kupoteza nguvu kazi ya Tifa.

Baraka amesema kampuni ya Codeban Company Limited ambayo ni kampuni ya kitanzania inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya usalama wa kazi imelenga kuwafikia wachimbaji wadogo wakati,wakubwa pamoja na wachenjuaji  mkoani Geita kwa lengo la kuwapa elimu juu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga wakati wa shughuli zao.

”Sisi kama kampuni ya Codeban tumepanga kwenda kuwatembelea wachimbaji wadogo wadogo na wachenjuaji kwenye planti zao  na kwenye migodi yao hii ni kuwapa elimu kwanini watumie bidhaa za kujikinga sehemu za kazi itasaidia kupata uelewa juu ya matumizi ya vifaa vya usalama kazini.

Kwa upande wake Eliwaza Mzonge Afisa mauzo pamoja na Hadija Swaleh Afisa masoko kutoka kampuni ya Kaka Chemicals Tanzania ambao ni wauzaji wa kemikali za migodini wamesema utumiaji wa kemikali migodini bila elimu sahihi unaweza kusababisha kuwa chanzo cha magojwa mbalimbali ikiwemo TB.

Wamezungumzia uamuzi wao wa kutumia fursa katika maonesho hayo ili kuwafikia wachimbaji wengi hasa waliopo katika mkoa wa Geita kwa kuwapa elimu sahihi juu ya matumizi ya kemikali zilizo bora migodini.

Wamesema wao kama kampuni ya Kaka Chemical wanauza kemikali zinazotumika migodini huku wakiwapa elimu juu ya matumizi sahihi ya kemikali hizo  katika shughuli zao kwa lengo la kuepukana na madhara yanayoweza kutokana na kemikali hizo.

Aidha Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Ofisi za Mkoa wa Geita, imewataka wafanyabiashara  pamoja na wajasilimali mkoani humo kuachana na dhana potofu juu ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Akizungumza katika maonesho yanayoendelea katika viwanja vya CCM kalangalala Ofisa Huduma Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Ofisi za Geita, James Katiti amesema VAT haiongezi gharama ya kodi bali inalipwa kwa thamani ya faida ya utoaji huduma kwa mteja.

“Niwaondoe hofu wafanyabaishara kwamba ukisajiliwa kwenye VAT kwamba kunaongeza gharama, (ya kodi) hamna gharama yeyote, sanasana inamupa nafasi mfanyabiashara atakapokwenda kunua bidhaa mfano pikipiki atakapokwenda kununua pikipiki atalipa VAT kule.

Katiti alitumia nafasi hiyo kuwataka wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara kwa miongozo ili  waweze kulipa kodi kwa serikali hali itakayo saidia juhudi za serikali kuboresha  miundombinu mbali mbali ya kimaendeleo.
Previous articleMBUNGE BONAH AFANYA ZIARA KWENYE BARABARA YA CHANG’OMBE-MACHIMBO
Next articleMADIWANI ILALA WAJIPANGA KWA SENSA YA MAKAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here