Wauguzi na wakunga wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wanakabiliwa na changamoto ya kutopata stahiki zao kwa wakati hali inayopelekea kusababisha kutotimiza majukumu yao kwa ufanisi na kuwapunguzia hali ya utendaji kazi katika majukumu yao.
Baadhi ya wauguzi na wakunga wameiomba Serikali wilayani humo kuwatatulia changamoto inayowakabili ya kucheleweshewa stahiki zao kwa wakati hali inayosababisha kutotimiza majukumu yao ipasavyo wawapo kazini.
Muuguzi mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Beatrice Munisi amesema licha ya upungufu na changamoto za wauguzi kwenye vituo vya Afya lakini wamekuwa wakitimiza majukumu yao kikamilifu.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo mganga mkuu wa wilaya ya Geita Dokta Modest Buchard amesema atahakikisha wauguzi na wakunga wanapata stahiki zao kwa wakati ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi.