Home LOCAL WAUGUZI NA WAKUNGA WILAYA YA GEITA WALIA NA STAHIKI ZAO.

WAUGUZI NA WAKUNGA WILAYA YA GEITA WALIA NA STAHIKI ZAO.

Na: Costantine James, Geita.

Wauguzi na wakunga wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wanakabiliwa na changamoto ya kutopata stahiki zao kwa wakati hali inayopelekea kusababisha  kutotimiza majukumu yao kwa ufanisi na kuwapunguzia hali ya utendaji kazi katika majukumu yao.

Baadhi ya wauguzi na wakunga wameiomba Serikali wilayani humo kuwatatulia changamoto  inayowakabili ya kucheleweshewa stahiki  zao kwa wakati  hali inayosababisha  kutotimiza majukumu yao ipasavyo wawapo kazini.

Muuguzi mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Beatrice Munisi amesema licha ya  upungufu na changamoto za  wauguzi kwenye vituo vya Afya lakini wamekuwa wakitimiza majukumu yao kikamilifu.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo mganga mkuu wa wilaya ya Geita Dokta Modest Buchard amesema atahakikisha wauguzi na wakunga wanapata stahiki zao kwa wakati ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi.

Previous articleSIMBA SC YAMTUPIA VIRAGO PABLO
Next articleRAIS SAMIA SULUHU APOKEA KOMBE LA DUNIA, AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA FURSA KUPITIA MICHEZO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here