Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Dkt. George S. Fasha kuhusu maboresho na miradi mbalimbali inayofanyika na inayoendelea kufanyika katika ukanda wa Bahari ya Hindi (Dar es Salaam, Tanga na Mtwara), pamoja na Maziwa Makuu (Kyela, Mwanza na Kigoma), wakati Mhe, Rais alipotembelea Banda la Mamlaka hiyo mapema yabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Wanawake na Vijana ulioandaliwa na Sekretarieti ya eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 12 hadi 14,2022 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni Afisa Mawasiliano wa TPA Omary Khalid.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Dkt. George S. Fasha (kustoto) akiwa katika picha ya pamoja wa na Maofisa wengine kutoka katika Mamlaka hiyo. (kutoka kushoto) ni, Afisa Mawasiliano wa TPA Omary Khalid, Maafisa Masoko Marietha kileo, pamoja na Glory Kisanga. (kulia)