Home BUSINESS RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA TIC KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE...

RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA TIC KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE NA VIJANA WA (AfCFTA) JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali (wa kwanza kulia) akielezea namna kituo hicho kinavyohamasisha Uwekezaji kwa wanawake na vijana sambamba na kutoa ushirikiano kwa makundi hayo wakati wanapotaka kufanya shughuli za uwekezaji.

Rais Samia alitembelea katika Banda la Taasisi hiyo mapema leo asubuhi kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Wanawake na Vijana ulioandaliwa na Sekretarieti ya eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 12 hadi 14,2022 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia) ni Afisa Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano TIC, Pendo Gondwe.

(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)

PICHA MBALIMBALI ZA MHE. RAIS SAMIA AKIWA KATIKA BANDA LA TIC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Maofisa wa TIC mara baada ya kupata maelezo katika Banda hilo.

Previous articleRAIS SAMIA ATEMBELA BANDA LA TPA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE NA VIJANA WA (AfCFTA)
Next articleRAIS SAMIA AHUTUBIA KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE NA VIJANA WA ENEO HURU LA BIASHARA LA AFRIKA (AFCFTA)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here