SERENGETI.
Katibu Muhtasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Vivian Valerian Malasha amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Serengeti akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi Namba 84 ya Mwaka 2022.
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), William Lyamboko alisema mbele ya Hakimu Jacob Ndira kwamba kupitia Kesi hiyo, Malasha anashitakiwa kwa makosa ya Ufujaji na ubadhirifu wa Sh milioni 2.160 kinyume na kifungu cha 28 (1) PCCA, kikisomwa pamoja na vifungu vya 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupanga CAP 200.R.E 2019.
Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana na kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa tena Julai 06 Mwaka huu.